ULANGA
NA Fatuma Mtemangani
Wanafunzi wa kidato cha pili na kidato cha nne shule ya sekondari ya Nawenge Wilayani Ulanga Mkoani Morogoro wamehimizwa kusoma kwa bidii,maarifa na kuongeza juhudi ili kuendeleza rekodi ya ufaulu katika mitihani ya taifa.
Akizungumza na wanafunzi na walimu wa shule ya nawenge sekondari afisa elimu sekondari ndugu Menard Lupenza amesema kua serikali imefanya jitihada ya kuboresha upande wa elimu kwa kuwapatia posho walimu wakuu na maafisa elimu kata ili waweze kufanya kazi bila kikwazo chochote.
Hata hivyo amesema kua kupitia mpango wa elimu bila malipo kwa wilaya ya ulanga shule ishirini na tisa zimepokea fedha za kujikimu na utaratibu wa matumizi unafanyika vizuri kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na serikali na hakuna changamoto yeyote katika shule hizo.
“Wanafunzi msome kwa bidii na kuwa na nidhamu ili baadae wawe madaktari,marubani waandishi wa habarin walimu wazuri na waweze kutimiza ndoto zenu kama mtasoma kwa bidii na kufuata sheria na taratibu za shule pia kuelewa kile unachofundishwa na walumu”.aalisema lupenza.
Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari Nawenge Bi.Setina Ngairo amewaahidi kuendeleza utaratibu wa kufanya vizuri katika mitihani hiyo na kusema kua hawata iangusha halmashauri ya wilaya ya ulanga hivyo atahakikisha walimu wanafundisha kwa bidii ili kupata matokeo mazuri.
Aidha mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Furaha Lilongeli amewataka viongozi kuwafikia wananchi kwa kuhamasisha wazazi na walezi kutoa ushirikiano kwenye shule husika ili wazazi hao waweze kuchangia nguvu kazi katika shule hizo hasa katika ujenzi wa vyumba vya madarasa,maabara,pamoja na nyumba za walimu kwa kuchangia matofali na kusomba mchanga ili ujenzi uweze kukamilika kwa wakati kwani viongozi ni chachu ya maendeleo katika kata,kijiji na kitongoji.
“Kwanza nawapongeza sana walimu,wanafunzi wote waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha nne na sita pamoja na wazazi kwa kutoa ushirikiano wao kwa walimu,pia mliobaki msome kwa bidii kwani halmashauri itaendelea kuwaboreshea mazingira mazuri ya kusomea na kujifunzia kwa kumalizia majengo ya maabara.”alisema mh.lilongeli.
Kambi ya kitaaluma ya shule ya sekondari nawenge ina jumuisha wanafunzi sitini wa kidato cha pili na nne kati ya hao wakiwemo wavulana arobaini na wasichana ishirini ili kujiandaa na mtihani wa taifa ambapo unatarajia kufanyika hivi karibuni.
MWISHO.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.