Na Yuster Sengo
Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga,limeagiza kusimamishwa kazi kwa watumishi 16 waliotajwa katika tuhuma za ubadhirifu wa fedha za halmashauri
Akizungumza katika kikao maalum cha baraza la madiwani Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga Mh Furaha Lilongelui amesema kuwa wamefikia uamuzi huo ili kujenga ustawi wa halmashuri hiyo
Aidha ameongeza kuwa ,haya yote yametokea baada kujadiliana suala hilo kwa kina kwa ushirikiano wa mbunge wa jimbo la Ulanga Mh.Goolack Mlinga pamoja na wajumbe akiwemo katibu tawala wa mkoa wa morogoro
“hayo ni maamuzi ya hekima ,busara na unyenyekevu yanayolenga kulinda masrahi mapana ya wananchi wa wilaya ya ulanga “alisema Mh Lilongeli
Mh Lilongeli ameongeza kuwa maamuzi yaliyochukuliwa ni kusimamishwa kazi kwa watumishi 16,vyombo vya dola viwachukulie hatua na vyombo vya uchunguzi viwachunguze na ikithibitka kama wamehusika na upotevu wa fedha wafikishwe mahakamani
“tumekaa katika baraza hili maalum na kukubaliana kuwachukulia hatua watumishi 16 waliohusishwa kwenye tuhuma za upotevu wa fedha zaidi ya shilingi bilioni mbili ,wasimamishwe kazi ,vyombo vya uchunguzi viwachunguze na wakibainika kama kweli wamehusika watafikishwa mahakamani na la zaidi watarudisha hizo pesa zilizopotea”amesema Mh Lilongeli
Hata hivyo Mh Lilongeli ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya yaulanga ,amewashukuru madiwani,mkuu wa wilaya ,mbunge wa jimbo la Ulanga na katibu tawala mkoa pamoja na wajumbe wengine walioshiriki katika maamuzi hayo
Maamuzi juu ya watumishi hao 16,yametokea baada ya kutokea kwa upotevu wa fedha zaidi ya shilingi bilioni mbili ambazo imeelezwa kuwa fedha hizo zimepotezwa na watumishi hao
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.