Na Jackson Machowa
Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya ulanga mkoani morogoro limepitisha ombi maalum la kuiomba serikali kuridhia kutowaondoa wananchi walioanzisha makazi ya kudumu na miundombinu mingine kama vile ya shule katika maeneo ya hifadhi.
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani kilichoketi kwa siku mbili mwishoni mwa juma lililomalizika mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya ulanga na diwani wa kata ya mwaya mh. furaha lilongeli amesema wataiomba serikali kutowaondoa wananchi walioanzisha makazi huku akisisitiza kuwa ni lazima wote waliopo katika kiini cha hifadhi waondolewe kwa maslahi mapana ya nchi.
“Hoja hapo labda kwenye hayo maeneo ya makazi lakini hakuna siasa katika hilo, mh rais amesema tumesikia kukisema tufanye siasa itakuja kuwa shida. amesema mh. lilongeri mwenyekiti wa halmashauri ulanga.
Kwa upande mbunge wa jimbo la ulanga mh. goodluck mlinga amesema mh. rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania dkt john pombe magufuli akiwa na mradi mkubwa wenye maslahi makubwa kwa taifa mtu yeyote atakaye kwamisha atachukuliwa hatua.
Ameongeza kuwa yeye alijaribu kuzuia bajeti ya wizara ya maliasili kwa kutaka hoja ya watu waliopo katika bonde wasiondolewe lakini alizuiliwa kuendelea na hoja yake kutoka na suala lililopo linamaslahi mapana kwa taifa.
“Mimi mwenyewe binafsi bungeni nilizuia bajeti ya wizara ya mali asili kwa kutaka hoja watu ambao wapo kwenye bonde kidole nilichooneshewa…….
“Rais wetu alivyo akiwa ana mradi mkubwa kwa maslahi makubwa kwa taifa yaani ukitia “kucha” yeyote yaani wewe unakuwa mbaya kwake.”
Awali waheshimiwa madiwani akiwemo mh. khatibu chitaunga na mh. madunda mkalimoto kutoka kata za lupiro na iragua ambao ni kata zilizopakana na bonde la mto kilombero wamesema wananchi wao hawana maeneo ya kilimo na umbali uliowekwa kutoka chanzo cha mto huo na walipo wananchi ni mkubwa.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.