Na.Yuster Sengo
Waziri wan chi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mh.Innocent Bashungwa amewaagiza viongozi wa sekretalieti za mikoa na mamalaka za Serikali za mitaa kuhakikisha wanawatumia maafisa habari katika kuhabarisha wananchi kuhusu kazi na miradi inayotekelezwa na serikali
Akizungumza wakati wa kikao kazi cha maafisa uhusiano wa Taasisi, Maafia Habari wa Mikoa na mamlaka ya Serikali za mitaa kilichofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa jijini Dodoma Mh. Bashungwa amewataka viongozi hao kuhakikisha wanawatumia maafisa habari waliopo kwenye maeneo yao kutangaza miradi ya maendeleo inayotekelezwa nchi nzima na serikali ya awamu ya sita
“Suala la kuhabarisha umma ni la kufa na kupona kuhusu utendaji kazi wa serikali kwa watanzania ni muhimu ,si jambo la hiari bali ni lazima kuhabarisha umma juhudi za serikali katika kuwatumikia wananchi “Amesema waziri Bashungwa
Hata hivyo amewataka wakuu wa Mikoa,Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya ,Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi katika mwaka wa fedha 2022/2023 kuhakikisha wanatoa habari kuanzia ngazi za kijiji,Mtaa,Wilaya Mikoa na Taifa kwa ujumla ili kila Mtanzania aweze kujua kazi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan
“hivyo basi nawaagiza viongozi hao kuhakikisha wanawasimamia Maafisa Habari wa mikoa na Serikali za Mitaa ili waweze kutimiza wajibu wao wa kuhabarisha umma wa wa Tanzania kwa kuzingatia utaratibu na sheria na miongozo ya utumishi wa umma “Ameongeza Mh.Bashungwa
Kwa upande wa Msemaji wa Serikali na mkurugenzi wa Habari maelezo Gerson Msigwa amewataka Maafisa Habari wote nchini kutumia Redio na Televisin za kijamii katika maeneo yao kutangazamafanikio na agenda ya Kitaifa ili kuweza kuisaidia Serikali
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.