ULANGA
NA YUSTER SENGO
Afisa matekelezo pia mratibu wa bima ya afya mkoa wa morogoro Bw.Hamidu Mwambungu amesema kuwa Bima ya afya ya NHIF na CHF iliyoboreshwa wanatarajia kujiunga kwa pamoja ili kuboresha wigo wa huduma za afya hapa nchini.
Bwana Mwambungu amesema kuwa lengo la kuungana na CHF iliyoboreshwa ni kuiboresha zaidi ili mwanachama aweze kupata huduma za afya kutoka katika vituo vya afya kwa nchi nzima tofauti na hapo awali.
Aidha ameongeza kuwa kutokana na kuboreshwa zaidi kwa CHF mwanachama atalipia shilingi elfu thelathini kwa mwaka badala ya shilingi elfu kumi kama ilivyokuwa hapo awali ambapo huduma hiyo ilikuwa ikitolewa katika mikoa mitatu tu ikiwemo mkoa wa Morogoro,Dodoma pamoja na Shinyanga.
Aidha Bw.Hamidu ameongeza kuwa mwanachama atapatiwa huduma zote za msingi na hivyo kuna baadhi ya huduma ambazo haziwezi kutolewa ukiwa na kadi ya CHF lakini maboresho bado yanaendelea kufanyika zaidi ili mwanachama aweze kupata huduma bora zaidi.
Akizungumzia huduma hizo zitakazoboreshwa zaidi amesema kua bima ya afya ya CHF itatoa huduma mbalimbali ikiwemo gharama za vipimo,gharama za dawa,gharama za nje na kulazwa..
Pia bima ya afya CHF itatowa huduma kwa watoto walio chini ya miaka kumi na nane kwani afya zao zikiteteleka katika umri mdogo hawataweza kuwa na afya nzuri yakuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi na ustawi wa taifa kwa jamii zinazowazunguka.
Aidha ameongeza kuwa wanatarajia kutoa elimu kwa wanachi wa wilaya ya Ulanga juu ya kujiunga na huduma hiyo na kuwataka wananchi kujiunga na huduma hii ili waweze kupata matibabu kwa wakati.
MWISHO.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.