ULANGA
NA YUSTER SENGO
Chama cha wanasheria wanawakeTanzania wameitaka jamii kushirikisha wanawake katika maamuzi na umiliki wa ardhi ili waweze kujikwamua kiuchumi
Hatua hiyi imekuja mara baada ya kubainishwa kuwa kundi la wanawake limekua ni wahanga wakubwa wanaowekwa mbali katika kumiliki ardhi na badala yake wanaume ndio wanaopewa kipaumbele hicho katika jamii mbalmbali
Akizungumza katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa halmashari wa wilaya ya ulanga ,mratibu wa mradi waurasimishaji ardhi Bi.Maria Mruma amesema kuwa mradi huu umetelekezwa katika wilaya mbili ambazo ni kilombero na ulanga,na katika wilaya ya ulanga tayari wameshatembelea vijiji kumi kwaajili ya kutoa elimu
Vijiji walivyotembelea ni pamoja na Iputi,mbuga,chilombora,chikuti,nalukoo,ketaketa ,ibuyi pamoja na igota na kufanikiwa kutoa elimu juu ya haki na wajibu kwenye umiliki wa ardhi ili kuongeza ushiriki mpana wa wananchi kwenye program ya upimaji na urasimishaji ardhi
Aidha Bi Mruma , amesema kuwa wanatarajia kuanzisha sheria ndogo za kijiji zinazoangalia jinsia hususani wanawake ili waweze kupewa kipaumbele katika umiliki wa ardhi kwani ni kundi linaloachwa nyuma katika suala hili
“katika vijiji tulivyopita wanawake wengi hawajihusishi kabisa katika vikao vinavyohusu mambo ya ardhi na sehemu nyingine unakuta wanawake wamekaa nje wnaendelea na shughuli nyingine ukiwauliza kwanini hawaendi kuhudhuria kikao wnasema mambo ya ardhi yanawahusu wanaume”Amesema Bi Mruma
Aidha ameongeza kuwa katika vijiji walivyopitia wametoa elimu ya sheria ya ndoa kwani wamegundua jamii walizotembelea hawana uelewa mkubwa katika sheria hiyo
”tumefundisha pia kuhusu sheria ya ndoa kwani tumeona wanawake wanadhurumiwa haki zao kwakutokujua sheria,mke na mume wakiamua kuachana mali walizochuma wakiwa pamoja inapaswa zigawanyishwe sawasawa lakini kwa sasa utakuta wakiachana mwanamke anatoka bila kitu na hii ni kwasababu yakutojua sheri na haki yake kama mwana ndoa”
Hata hivyo Bi.Mruma ameongeza kuwa ni vizuri jami kwa ujumla ikafanya jitihada ya kumshirikisha mwanamke kumiliki ardhi iwe kwa kununua yeye mwenyewe,kurithi kutoka kwa wazazi au hata kurithi kutoka kwa mume.
MWISHO
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.