Na.Yuster Sengo
Wataalam wa wizara ya Mali asili na utalii wamefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga kwa lengo la kushirikiana na wilaya hiyo na kuhakikisha kuwa Halmashauri ya Ulanga inamiliki msitu wa hifadhi kwani suala hilo ni la kisheria
Akizungumza mara baada ya kikao cha wataalamu wa wizara na wakuu wa idara na vitengo vya Halmashauri ,Afisa Misitu mkuu Bw. Seleboni John amesema kuwa sheria inatambua kuwa Halmashauri yoyote nchini inaweza kumiliki msitu wa hifadhi ili kuweza kuongeza mapato ya Halmashauri husika
“Sheria inatambua kuwa Halmashauri inaweza kumiliki msitu kwa kuwa Halmashauri inaweza kupata kipato kwa kupitia rasilimali za misitu lakini pia inaweza kuendeleza juhudi za kihifadhi katika kuhakikisha kwamba uharibu wa misitu unapungua na uvunaji wa misitu unaendelea katika misingi ambayo ni endelevu “Amesema Bw. Seleboni John
‘kuhifadhiwa kwa misitu kuna faida nyingi ikiwa ni pamoja na miradi mikubwa amabayo inaendelea kwa sasa kama mradi wa bwawa la Mwl Nyerere na pia uhifadhi wa misitu unatusaidia katika kuleta mvua na kuondoa changamoto ya mabaidiliko ya hali ya hewa”Ameongeza Bw.Seleboni
Aidha ameongeza kuwa Halmashauri ya wilaya ya Ulanga imefanya juhudi kubwa ya kuhakikisha inamiliki na kusimamia msitu wa Halmashauri ambapo kwa hatua ya kwanza imeshaandaa mpango wa usimamizi,imefanya tathmini ya Rasilimali na kushirikisha vijiji saba vinavyozunguka msitu huo pamoja na kutoa elimu ya kutosha kwa jamii inayozunguka msitu huo
Hata hivyo amesema kwamba kwa sasa hatua iliyofikiwa ni kuandaa notisi ya serikali kwaajili ya wadau wengi zaidi kushirikishwa ili kama kuna mtu mwenye pingamizi aweze kulitoa
“kama kuna mtu atakuwa na pingamizi basi kwa hatua hii anaweza kutoa pingamizi hilo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri atapeleka hayo mapingamizi yaliyojitokeza Wizara ya Maliasili na Utalii ili wizara iendelee na taratibu za kukamilisha Halmashauri kumiliki Msitu”Amesa Bw. Seleboni
Akizungumza wakati wa kikao hicho Afisa Misitu wilaya ya Ulanga Bi. Florencia Massawe amewashukuru wataalam kutoka wizara ya maliasili kwa kuja kuangalia mchakato unavyoendelea na elimu waliyotoa wakati wa ziara yao
‘’Tunashukuru sana kwa Elimu mliyotupa kuhusu umiliki na usimamizi wa msitu ,naomba muendelee kutuongoza na kutushauri ili tuweze kufika pazuri na hata wakati wa kuandaa tangazo tunaomba ushirikiaano wenu ili tutoe tangazo zuri lililo beba vitu vyote vya msingi”Amesema Bi.Massawe
Mwisho
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.