NA YUSTER SENGO
Kufuatia matokeao ya kidato cha nne 2018, wilaya ya ulanga imeshika nafasi ya pili kimkoa na nafasi ya thelathini kitaifa ambapo ufaulu huo umeongezeka ukilinganisha na mwaka 2017 ambapo ufaulu huo umeongezeka kwa asilimi 1.61
Afisa elimu Bw.Menrad Lupenza amesema kuwa mwaka 2018, jumla ya wanafunzi 1236 wilayani hapa walifanya mtihani wa kumaliza kidato cha nne 2018 ikiwa wanafunzi waliofanya mtihani wa kujitegemea ni 63 na wanafunzi wa shule za sekondari 1173
Pia wanafunzi 30 waliofanya mtihani wa maarifa yaani QT, ambapo wanafunzi 10 wamefaulu mtihani huo wa maarifa na wafunzi 20 wamefeli mtihani huo hivyo ufaulu huu kwa wanafunzi wote waliofanya mtihani ni sawa na asilimia 85.85
Aidha ameongeza kuwa kwa mwaka huu wa 2018, GPA imependa katika halmashauri ya wialaya ya ulanga ambapo kwa mwaka 2017 GPA ilikuwa 3.876 na kwa mwaka 2018 GPA imepanda kwa 3.73 ambapo amefafanua kuwa kwa udogo wa GPA maana yake ni kuwa ufaulu umeongezeka
Sambamba na hayo Bw Lupenza amesema kuwa kimkoa halimashauri ya wilaya ya ulanga Imeshika nafasi ya pili kwa jumla ya wila 9 na kitaifa wilaya hiyo imeshika nafasi 30 kwa jumla ya Halimashauri 195 hivyo nakuonekana wilaya imefanya vizuri.
Licha ya kupanda kwa ufaulu wilayani hapa, Afisa elimu Bw Lupenza ameongeza kuwa wanafunzi wapate mazoezi ya kutosha na kudhibiti nidhamu hivyo wazazi washilikishwe katika malengo ya shule na maendeleo ya wilaya kwa ujulma kwa kutoa michango ya chakula na kufanya maendeleo ya watoto wao lakini pia walimu wafuatilie na kuhakikisha wanawafatilia wanafunzi ili kuhakikisha wanaondoa sifuri mashuleni
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.