Na Yuster Sengo
Ikiwa leo ni siku ya kilele cha upandaji miti kitaifa, wilaya ya Ulanga imeadhimisha siku hiyo kwa kupanda miche ya miti zaidi ya 300 katika kijiji cha mbagula wilayani hapa
Akizungumza katika maadhimisho hayo ,Afisa tawala Bi Huruka Rajab ambaye alimuwakilisha mkuu wa wilaya ya Ulanga Mh.Ngollo Malenya, amewataka wakazi wa kijiji cha Mbagula kitongoji cha ukwama kulinda na kuitunza miti hiyo ili ilete faida kwa vizazi vya sasa n avya baadae
Aidha ameongeza kuwa katika utunzaji wa mazingira ,tunaweza tukaboresha viwanda vyetu kwakuwa viwanda vya mbao au miti vinakazi nyingi sana ambapo tunategemea kupata vitu mbali mbali kutoka katika miti
“Tuitunze miti hii tunayoipanda leo kwakuwa inaweza kutuletea faida mbalimbali ikiwa ni pamoja na mbao,karatasi,vibiriti,thamani za ndani kutoka viwandani ,hivyo ni jukumu la kila mtu kutunza mazingira na kutunza miti yetu”,Amesema bi Huruka
Aidha ameongeza kuwa miti imekuwa ni chanzo kizuri cha mvua na hali ya hewa nzuri lakini pia inasaidia katika majanga mbali mbali kama vile mafuriko na ukame hivyo hatuna budi kuitunza ili pia kuweza kufikia lengo la Halmashauri ya wilaya ya Ulanga ya kuwa na miti milioni moja na laki tano kila mwaka.
“Hivyo niwasisitize wanambagula,viongozi na mwenyekiti pamoja na serikali yako ya kijiji mtunze miti inayopandwa leo kwasababu kila mmoja wenu hapo anajua umuhimu wa miti na kutunza mazingira ,na ndiyo maana siku zote tunakumbushwa kuwa tutunze mazingira ili nayo yatutunze”Ameongeza Hurka
Naye mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Bw. Mohamed Atiki ambaye alikuwa anamuwakilisha mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga amesema kuwa takwimu zinaonesha kuwa kila kaya inatakiwa kupanda miti isiyopungua elfu 20 ili kufikia lengo la kiwilaya hivyo kuwataka wakazi wa ukwama kuilinda miti hiyo ili iweze kuleta tija hapo baadae
Hata hivyo mkuu wa idara ya mazingira Bw. Justine Bundu,amesema kuwa katika kilele cha upandaji miti kitaifa ,wilaya ya Ulanga imepanda miti zaidi ya 150, wakati kiwilaya tunatakiwa kupanda miti milioni moja na laki tano na kwa mujibu wa idadi ya vijiji tulivynavyo wanatakiwa kupanda miti elf 20 kwa kila kijiji
Aidha ameongeza kuwa idara yake imeshaanza kupokea takwimu tangu zoezi lianze mpaka sasa hivi miti iliyopandwa ni zaidi ya miti laki nne,na kwa miaka miwili ya nyuma tumeweza kupanda miti kwa asilimia tisini kwa 2016/2017 na mwaka 2018/2019 tumepanda kwa asilima 89 na kwa mujibu wa takwimu tulizokusanya ,asilimia zaidi ya sabiniimepona.
Hata hivyo tunategemea jukumu kubwa lausimamizi wa miti hii ni kutoka kwa viongozi wa kitongoji cha ukwama pamoja na wananchi kiujumla kuisimamia kwa ukaribu zaidi
“kuna changamato za usimamizi wa miti inayopandwa na ndiyo maana kwa sasa mikakati ya wilaya ni kupanda kwenye taasisi, maana miaka ya nyuma tulikua tunapanda sehemu za wazi lakini tukiondoka tu miche hiyo inaliwa na mbuzi na inaharibika lakini kwa kupanda kwenye taasisi tunaimani wahusika wataitunza vizuri “amesema Bundu
Maadhimisho ya siku ya kilele cha upandaji miti kitaifa,imeongozwa na kauli mbiu isemayo “TANZANIA YA VIWANDA INAWEZEKANA ,PANDA MITI KWA MAENDELEO YA VIWANDA
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.