Na.Yuster Sengo
Halmashauri ya wilaya ya Ulanga imepanga kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 28(28,434,490,700.00) katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019 -2020 hii ikiwa ni mapato ya ndani ya halmashauri ambapo hadi kufikia desemba 31 2019 halmashauri ilikua imekusanya zaidi ya shilingi bilioni moja(1,471,405,012.99) sawa na asilimia 59 ya makusanyo kwa mwaka
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa halmashauuri ya wilaya ya Ulanga Mh.Nassoro kihiyo wakati akisoma hotuba ya ufunguzi wa kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika tarehe 26 february 2020 katika ukumbi wa halmashauri hiyo Pauline hall
Aidha ameongeza kuwa kwa robo ya pili inayoishia December 31, halmashauri ya wilaya ya Ulanga imekusanya zaidi ya shilingi milioni miatano (500,060,997.00) sawa na asilimia 80.36 ya lengo la makusanyo kwa robo ya pili
Hata hivyo ameongeza mapato ya ndani ya halmashauri yanaendelea kushuka kwasababu mbali mbali ikwemo kufungwa kwa mageti pamoja na kuisha kwa msimu wa baadhi ya mazao ikiwemo ufuta na mpunga na pia mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha
Akiendelea kusoma hotuba hiyo Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga Mh. Nassoro kihiyo amesema kuwa halmashauri ya wilaya ya ulanga imekumbwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ambapo mafuriko hayo yamesababisha madhara katika makazi ya watu ambapo hadi kufikia tarehe 31 january nyumba zipatazo 32 zimezingirwa na maji , miundombinu ya barabara imeharibika na hekali zaidi ya elfu tatu za mazao ya mahindi ,mpunga na ufuta zimeathiriwa
Kutokana na hali hiyo Mh. Nassoro amewataka madiwani pamoja na wajumbe wa kikao hicho kuendelea kuwashauri wananchi kupanda mazao ya mizizi hususani mihogo pamoja na kulima mazao ya mahindi kwenye maeneo ya miinuko na mpunga kwenye maeneo ya bondeni
Aidha amewata madiwani pamoja na wataalamu kuongeza usimamizi katika ukusanyaji wa mapto na kuwa wabunifu katika kubuni vyanzo vipya vya mapato vyenye uhalisia na tija vitakavyoleta maendeleo na ustawi wa jamii ya watu wa Ulanga na hlmashauri kwa ujumla
Hata hivyo ameongeza kuwa ili halmashauri iweze kujiimarisha kiuchumi anawaomba wananchi kulima mazao ya biashara kama vile korosho,pamba ,ufuta ,karanga miti na kokoa ili kuongeza kipato cha mwananchi mmoja mmoja na hatimae kupandisha mapato ya halmashauri
Mh. Nassoro amehitimisha kwa kusema kuw licha yakuwa na changamoto katika halmashuri hiyo ila kuna mafinikio ambayo imeipata katika kipindi cha robo ya pili Oktoba mpaka Desemba cha mwaka wa fedha 2019 / 2020 ikiwa ni pamoja na kupokea kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni mbili(2,300,759,553.25) zilizoidhinishwa na bajeti ya bunge kwaajili ya miradi ya maendeleo
Aidha ameongeza zaidi ya shilingi milioni mia nane(841,294,228.00) zimetengwa ikiwa ni 40% ya makusanyo ya ndani ya halmashauri ,na shilingi milioni mia mbili ishirini na nne(224,647,975.25) zimeelekezwa katika miradi ya maendeleo ikiwemo soko la mahenge mjini,stendi ya lupiro, sekondari ya selina kombani pamoja na mikopo ya wanawake na vijana na watu wenye ulemavu ,na asilimia 20 utekelezaji miradi vijijni zimepelekwa zaidi ya shilingi milioni mia moja ((149,765,316.65) katika vijiji 59 vya wilaya ya Ulanga
Mwisho
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.