Halmashauri ya wilaya ya Ulanga imepongezwa kwa kupata hati safi kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
Hayo yamebainishwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa Noel Kazimoto wakati akizungumza na Waheshimiwa madiwani katika kikao cha robo ya nne ya mwaka kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri Pauline.
Kazimoto pia amewapongeza halmashauri hiyo kwa kushirikiana na watendaji pamoja na wananchi kwa kufanikisha kupata hati safi na kushika nafasi ya tatu kwa mkoa wa Morogoro.
Hata hivyo amewataka waheshimiwa madiwani na watendaji wa vijiji kuongeza bidii kwa kushirikiana na wananchi ili kuziba maeneo yaliyoachwa kwa lengo la kuendelea kupata hati safi kwa wilaya ya Ulanga.
Aidha ameongeza kua kupitia kikao hicho waheshimiwa madiwani kwa dhamana waliyopewa na wananchi wanatakiwa kuwasaidia kutekeleza changamoto zinazowakabili pamoja na miradi ya maendeleo ya kata kwa wakati.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.