ULANGA
NA FATUMA MTEMANGANI
Halmashauri ya wilaya ya ulanga mkoani morogoro kupitia idara ya maji imewaagiza viongozi wa jumuiya za watumiaji maji kufika katika ofisi za idara ya maji kuchukua dawa aina ya krolini kwa ajili ya kutibu maji yanayoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali.
Akizungumza na ulanga fm ofisini kwake mwandisi wa maji wa wilaya ya ulanga bwana david kaijage amekiri kuwa mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali zinaathiri vyanzo vya maji hivyo kama halmashauri inajitahidi kudhibiti hali hiyo.
Aidha bwana kaijage amesema hali ya upatikanaji wa maji wilayani hapa bado imeendelea kusalia kuwa ni asilimia 59 ambapo wananchi wanalazimika kufuata maji hayo kwa umabli wa mita 400 huku akikiri uwepo wa changamoto mbalimbali na kuahidi kwamba serikali inazishughulikia.
Hata hivyo mhandisi amebainisha changamoto zinazoikumba idara ya maji ni pamoja na miundombinu ya maji kuharibika pamoja na watumiaji wa maji kulipia kiasi kidogo ambacho akiendeni na huduma inayotolewa.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.