Na .Yuster Sengo
Afisa tarafa ya vigoi bw Shabani Kiduta ameseama kuwa mheshimiwa rais wa jamhuri ya mungano wa tanzania anafanya juhudi kubwa za kupambana na kupunguza vifo vya kina mama na watoto kwa kuboresha huduma za afya hapa nchini
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya ulanga kwenye kikao kazi cha sekta ya afya kilichofanyika ukumbi wa udeko afisa tarafa huyo amesema kuwa mh rais ameitambua sekta ya afya kuwa ni muhimu na kuwataka wadau hao kumuunga mkono kwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa
“Mh Rais amewaka kipaumbele kikubwa katika sekta ya afya ili kupunguza vifo vya wakina mama na watoto hivyo sisi tuliopewa jukumu la kutoa huduma za afya kwa wananchi tujitahidi kufanya kazi kwa weledi ili kufikia hatua ya kufuta hivyo vifo kabisa ”Amesema Kiduta
Kiduta ameseama kuanzia mh rais aingie madarakani kwa miaka minne ameshajenga vituo vya afya ziadi ya 352 hii ikiwa ni kupambana vifo ya watanzania na kuwapatia huduma kwa ukaribu zaidi
Kikoa kazi hicho hufanyika kila robo kwa kujadili changamoto mbalimbali na mafanikio katika sekta ya afya hususani watoto,wakina mama na akina baba
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.