Ulanga
Na
Fatuma Mtemangani
Katibu tawala Wilaya ya Ulanga bwana Abrahamu Mwaikwira amesema kua ofisi ya mkuu wa wilaya imeona kuwa hatua za kisheria zikichukuliwa kwa baadhi ya watendaji itakuwa ni fundisho kwa wengine hivyo mwenyekiti wa Halmashauri anatakiwa kulitazama suala hilo na kuchukua hatua stahiki.
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani bwana Mwaikwira amesema ofisi ya mkuu wa Wilaya itawachukula hatua kali za kisheria kwa watendaji waliohamishwa vituo vya kazi kwa kusababisha uharibifu wa makusudi wa mifuko ya saruji iliyopelekwa katika maeneo yao kwa lengo la kutumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa.
“Mwenyekiti wa Halmshauri kupitia baraza lako la madiwani naomba ulitazame hilo kwa jicho la tatu na uchukue hatua kali kwa mtendaji yeyote atakaefanya ubadhilifu wa mali za Halmashauri kwa makusudi kwani tukilifumbia macho litatugharimu na inaturudisha nyuma kimaendeleo”Alisema Mwaikwira.
Kutokana na ongezeko la ufaulu wa mitihani ya darasa la saba Wilayani Ulanga imeshika nafasi ya kwanzaa kwa mkoa wa morogoro na nafasi ya 16 kitaifa hivyo kufanya kuwe na idadi kubwa ya wanafunzi watakaojiunga na elimu ya sekondari kwa mwaka 2019.
Aidha ufaulu huo umepelekea upungufu wa vyumba vya madarasa,viti pamoja na meza kwa wanafunzi watakaojiunga kidato cha kwanza hivyo watendaji wanapaswa kusimamia majukumu yao kwa kuzilinda mali za Halmashauri katika kata zao .
Mwisho.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.