Na.Musa Ngaluma
Halmashauri ya wilaya ya Ulanga imetenga kiasi cha shilingi milioni 30 kwaajili ya machinjio yaliyopo katika kitongoji cha kisiwani kata ya uponera wilayani ulanga mkoani morogoro ambayo yapo katika hali mbaya kwa sasa
Hayo yamesemwa na kaimu afisa mifugo Bw. Juma kapilima alipokuwa akizungumza na ulanga fm,kuhusu malalamiko ya wakazi wa eneo hilo wanaolalamikia hali mbaya ya machinjio hayo yanayotishia kuhatarisha afya zao
”Kweli nakubali changamoto hizo zipo na serikali imepanga kiasi cha shilingi million 30 kwaajili ya ukarabati ila tunachongoja ni hizo pesa zitufikie ili tuanze ukarabati huo ila kwa sasa tutafanya marekebisho yasiyo hitaji pesa ili kero hizo ziweze kupungua katika eneo hilo”Amesema Bw.Kapilima
Kwa upande wa wakazi wa eneo hilo wakizungumza katika mkutano mkuu wa kijiji cha uponera wamesema kuwa wapo hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu,na magonjwa ya tumbo kutokana na kuzagaa kwa nzi na harufu mbaya inayotoka katika maeneo ya machinjio hayo hasa wakati wa jioni
Hata hivyo wananchi hao wameomba viongozi wa serikali hususani viongozi wa afya kutembelea eneo la michinjio hayo na kujionea ilipo kwa sasa ili kutafuta njia ya kutatua tatizo hilo
Mwisho
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.