Timu ya jeshi la Magereza yaifunga timu ya Waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga goli moja kwa sifuri katika mchezo wa kirafiki uliofanyika hivi karibuni.
Goli hilo lilifungwa na Nurdin Mrope aliyekwamisha wavuni mpira baada ya kazi nzuri iliyosukwa na Stamili Shaabani mnamo dakika ta 12 katika kipindi cha kwanza.
Timu ya madiwani ilijitahidi kuhakikisha wanarudisha goli hilo lakini washambuliaji wa madiwani wakiongozwa na Mh.Madunda Mkalimoto walizuiliwa vilivyo na safu ya ulinzi ya timu ya Magereza ambayo ilitumia wachezaji chipukizi.
Kipindi cha pili kilikuwa kigumu zaidi kwa timu ya Madiwani kwani isingekuwa ni juhudi binafsi za golikipa namba moja wa timu hiyo Mh. Michael Mahiringa aliyeokoa mikwaju kadhaa ya hatari langoni kwake.
Kocha wa timu ya Madiwani Abdalah Mbumi alifanya mabadiliko kadhaa kipindi cha pili kwa kuamua kumtoa Mh Novatus Majiji na nafasi yake kuchukuliwa na Mh.Msalam Mohamed Msalam lakini mabadiliko hayo hayakuzaa matunda yeyote.
Msambuliaji tegemezi wa Magereza Nurdin Mrope ambaye ni mfungaji wa bao la kwanza alioneshwa kadi nyekundu dakika za majeruhi baada ya kumchezea rafu mbaya mchezaji wa timu ya Madiwani Hatibu Chitaunga .
Katika mchezo huo timu ya Magereza imezawadiwa ungo wa Azam Tv utakaowasaidia wafungwa kuangalia vipindi malimbali ikiwemo vipindi vya michezo ambapo mgeni rasmi wa mchezo huo alikuwa ni mwakilishi wa mkuu wa mkoa Ndugu Noel Kazimoto.
Mechi ya Wahesimiwa madiwani na jeshi la Magereza ulifanyika katika mji wa Mahenge ukiwa ni mchezo wa kudumisha mahusiano kati ya taasis hizi.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.