Mafunzo ya Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma Tanzania kwa Maafisa Habari,Maafisa Tehama yameanza hapo jana Mkoani Morogoro katika ukumbi wa Edema Hotel huku ikijumuisha mikoa mitano ikiwemo mkoa wa Tanga,Dododma,Arusha,Manyara pamoja na Morogoro,na yanatarajia kumalizika tarehe 23/03/2018.
Mkurugenzi msaidizi habari maelezo ambaye ni mgeni rasmi katika mafunzo hayo ndugu Rodney Thadeus amesema kuwa Maafisa habari na Maafisa Tehama wa Halmashauri mbalimbali hapa nchini wanatakiwa kutoa habari zenye uhakika ambazo hazitamchosha msomaji.
Ndugu Rodney Thadeus amesema kua Maafisa Habari wamebeba dhamana kubwa kwa Serikali hivyo wanatakiwa kutoa taarifa sahihi katika Halmashauri husika ili kuondoa usumbufu kwa wananchi juu ya kupata habari za Halmashauri zao.
“Ili kuboresha maendeleo ndani ya Halmashauri na kuisaidia nchi yetu iweze kusonga mbele na wananchi wapate taarifa za Halmashauri kwa wakati Maafisa Habari unapaswa kumshauri Mkurugenzi Mtendaji wako katika swala la maendeleo kupitia miradi yote ya Halmashauri”alisema ,mkurugenzi msaidizi Thadeus.
Hata hivyo Maafisa Habari na Maafisa Tehama wanapaswa kumshauri mkurugenzi wao katika swala la utekeiezaji wa miradi yote maendeleo iliyo ndani ya Halmashauri na pia kutumia njia ya mitandao,vyombo mbali mbali vya habari ikiwemo Redio,Magazeti,Majalida,Luninga,Mbao za Matangazo ya Halmashauri katika ngazi ya kata na kijiji,sokoni,Viwanja vya Mpira pamoja na “Kijiweni” ili kufikisha taarifa kwa haraka zaidi.
Lengo ni kuboresha Tovuti za Halmashauri kwa kuwapatia wananchi matukio mbalimbali,shughuli za maendeleo wanazopaswa kushiriki na utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Mwisho.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.