Maofisa tehama na mawasiliano wameagizwa kuhakikisha kila mwisho wa wiki wanaweka taarifa mpya kwenye tovuti za halmashauri zao.
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa habari na maelezo dk.hassan abasi ametoa agizo hilo wakati alipotembelea mafunzo kwa maofisa habari na tehama wa halmashauri na mikoa ya morogoro, kilimanjaro, arusha na tanga machi 24, 2017 mkoani morogoro yanayoendeelea katika ukumbi wa edema mkoani morogoro.
Dk. Hassan abasi amewataka maafisa hao kufanya kazi kwa weledi hivyo ifipofika ijumaa tarehe 25/3/2017 tovuti ya kila halmashari na mkoa iwe na taarifa mpya na ielezee shughuli zote zinazotendeka ndani ya halmashauri husika na wananchi waipate kwa wakati na uhakika.
Hata hivyo amesema kuwa moja ya haki ya kikatiba waliyonayo wananchi ni haki ya kupata taarifa, hivyo kwa kutotoa taarifa zilizo sahihi na kwa wakati wananchi watakuwa wamenyimwa na kukoseshwa haki yao ya kikatiba, hivyo kila ofisa aliyehudhuria mafunzo haya ahakikishe anawapa wananchi wake haki yao na kwa wakati.
Aidha serikali ya awamu ya tano yam h.dk.john pombe magufuli ina mipango mizuri kutokana na uchumi na viwanda ili wananchi wapate unafuu wa maisha hivyo amezitaka wilaya zote nchini kutekeleza miradi ya halmashauri ili zilete maendeleo.
Mwisho.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.