MVUA ZILIZO NYESHA TAREHE 28 MWEZI WA PILI MWAKA 2017 MPAKA TAREHE 1 MWEZI WA TATU ZIMESABABISHA KAYA ZAIDI YA ELFU NANE KUKUMBWA NA MAFURIKO KATIKA WILAYA YA ULANGA MKOANI MOROGORO KUKOSA MAHALI PA KUISHI.
HAYO YAMEBAINISHWA NA MKUU WA WILAYA MH.JACKOB KASEMA AMBAYE NI MWENYEKITI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA WAKATI ALIPOTEMBELEA KAYA PAMOJA NA MASHAMBA YALIYO KUMBWA NA MAFURIKO.
MH.KASEMA AMEONGEZA KUA MVUA HIZO ZILIZONYESHA MNAMO TAREHE ISHIRINI NA NANE MWEZI WA PILI NA TAREHE 1 MWEZI WA TATU MWAKA ELFU MBILI NA KUMI NA SABA NA KUSABABISHA MADARAJA MATANO{5}PAMOJA NA BAADHI YA MASHAMBA KUSOMBWA NA MAJI IKIWEMO MAZAO YA MPUNGA,MAHINDI PAMOJA NA UFUTA.
VIJIJI VILIVYO KUMBWA NA MAFURIKO HAYO NI PAMOJA NA KIJIJI CHA SALI,ISYAGA,EUGA,CHILOMBORA PAMOJA NA MGOLO
HATA HIVYO AMEWATAKA WAKULIMA KUA NA UVUMILIVU KWA KIPINDI HIKI CHA MATATIZO WAKATI SERIKALI IKIWA INASHUGHULIKIA SWALA HILO BAADA YA KUFANYA TATHIMINI NA KUJIRIDHISHA NA SASA TAARIFA HIZO TAYARI ZIMESHA FIKISHWA KATIKA OFISI YA MKUU WA MKOA KWA KUPATIWA UFUMBUZI.
AIDHA AMEWATAKA WANANCHI HAO KULIMA MAZAO YANAYOENDANA NA HALI YA HEWA IKIWE MAHINDI YANAYO KOMAA KWA MUDA MFUPI AINA YA SITUKA,VIAZI VITAMU PAMOJA NA MIHOGO ILI KUONDOKANA NA GANGA LA NJAA.
MWISHO.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.