ULANGA
Na
Fatuma Mtemangani
Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilayani Ulanga imemuhukumu kifungo cha miaka miwili jela bwana Americk Makoronja kwa kosa la wizi wa kuaminiwa kinyume na kifungo no 273(b) kanuni ya adhabu sura namba 16 iliyo fanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Akisoma mashitaka hayo mbele ya hakimu Mfawidhi Mh. Bi.Martha Mahumbuga , mwendesha mashitaka wa polisi inspecta Simon Mgonja amesema kua mnamo tarehe 06/06/2017 majira ya saa nane mchana mlalamikaji alimkabidhi mshitakiwa fedha tasrimu kiasi cha 400,000 ili atengeneze sofa seti moja lakini mshitakiwa hakufanya hivyo.
Aidha mshitakiwa alivyo somewa shitaka hilo mbele ya mh.Hakimu Bi. Martha Mahumbuga mshitakiwa alikili kosa hilo na ndipo mahakama ikamwadhibu kwa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka miwili jela.
Katika hatua nyingine mahakama ya Wilaya ya Ulanga imepanga kuanza kusikiliza kesi inayo mkabili bwana Wiliam Kamando anae tuhumiwa kuhusika na na makosa matatu ya kuchoma nyumba moto na kujeluhi shitaka ambalo litaanzwa kusikilizwa tarehe 06/02/2018.
Muendesha mashitaka wa polisi inspekta Mgonja ameieleza mahakama kwamba upelelezi umekamilika huku upande wa mashitaka wana mashahidi sita na vielelezo vitatu.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.