Na.Yuster Sengo
Waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa tanzania mh. kasim majaliwa ameagiza kusimamishwa kazi na kufikishwa mahakamani watumishi nane wa halmashauri ya wilaya ya ulanga kufuatia tuhuma za ubadhilifu wa fedha zaidi ya shilingi bilion moja
Wazirimkuu amechukua uamuzi huo septemba 16 mwaka huu alipotembelea wilayani ulanga mkoani morogoro ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake mkoani morogoro ikiwa na lengo la kukagua miradi ya maendeleo.
Akizungumza katika kikao cha watumishi wa halmashauri wa wilaya ya ulanga mh. majaliwa amesema kuwa watumishi hao wanaotuhumiwa kwa ubadhilifu warudishwe wilayani na kufikishwa mahakamani pia amewataka watumishi wa halmashauri ya wilaya ya ulanga kuacha kujiamulia kutumia fedha ya serikali iliyotengwa kwaajili ya miradi ya maendeleo hali inayochafua watumishi wengine na halmashauri kiujumla
“kuna baadhi ya watu katika halmashauri ambao siyo waaminifu lakini pia nimebaini wapo wengi tu miongoni mwenu ambao ni waadilifu katika utendaji,sasa hawa wachache wanaharibu sifa ya halmashauri hii”amesema waziri mkuu
Aidha waziri mkuu amesema kuwa watumishi hao nane ndio waliosababisha upotevu wa shilingi bilioni 1.14 ambazo zilitumika nje ya utaratibu
Waziri mkuu amewataja watumishi hao kuwa ni aliyekua mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ulanga Yusufu Semguruka,Rajabu Siriwa ambaye alikua mweka hazina wa halmashauri,Stanley Godwill aliyekua mkusanyaji mapato na Evans Mattilya ambaye alikua ni muhasibu
Wengine ni Isack Mwansankope na Johnson Mwanyobole ambao ni wahasibu ,Said Majaliwa ambaye ni mtaalam wa mifumo na Charles Eman ambao wote ni watumishi wa halmashauri hiyo
Aidha ameongeza kuwa atatuma timu kutoka tamisemi kwa ajili ya kuwafungulia mashtaka ili kukwepa kufunguliwa mashitaka mepesi na kuonekana suala hili ni la mchezo
Wakati huo huo waziri mkuu ameagiza kupewa ukuu wa idara kwa aliyekuwa kaimu mkaguzi wa ndani bw, Agusta mwaria ambaye pia alifanikisha kugundulika kwa upotevu wa fedha hizo ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni moja za halmashauri ya wilaya ya ulanga .
Mara baada ya kuongea na watumishi wa halmashauri ya Ulanga ,waziri mkuu alihutubia mkutano wa hadhara na kusikiliza kero za wananchi huku akimsifia mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe kwa kuimarisha mfuko wa bima ya Afya ulioboreshwa CHF kwakuweka utaratibu wa kila kaya yenye jumla ya watu sita kulipia shilingi elfu Thelathini hivyo kuwawezesha kutibiwa popote ndani ya mkoa
Ziara ya waziri mkuu bado inaendelea katika mkoa wa Morogoro ambapo tarehe 17 atakua katika wilaya ya Kilosa na baadae ataelekea katika halmashauri ya wilaya ya Morogoro
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.