JANUARI 19/1/2017 SAA 3:00USIKU USHIRIKIANO.
WAZAZI WILAYANI ULANGA MKOANI MOROGORO WAMETAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA SERIKALI PAMOJA NA WADAU MBALIMBALI KATIKA MALEZI YA WATOTO WAKIKE ILI KUTOKOMEZA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI MASHULENI.
AKIZUNGUMZA NA ULANGA FM MKUU WA SHULE YA SEKONDARI YA UPONERA BI JANETY MWANGUSI AMESEMA KUA WAZAZI WANATAKIWA KUIENZI KWA VITENDO KAULI YA NIACHE NISOME ILIYO ASISIWA NA ALIYEKUWA MKUU WILAYA YA ULANGA BI CHRISTINA MNDEME KWANI INAMCHANGO MKUBWA KATIKA KUKABILIANA NA MIMBA PAMOJA NDOA ZA UTOTONI MASHULENI ILIM KUSAIDIA WATOTO WA KIKE KUFIKIA MALENGO YAO.
BI MWANGUSI AMEONGEZA KUWA KAULI MBIU YA NIACHE NISOME IMEFANIKIWA KUSAIDIA KWA KIASI KIKUBWA KATIKA KUTOKOMEZA MIMBA UTOTONI NA NDOA ZA UTOTONI AMBAPO KWA KIPINDI CHA MWEZI JANUARI HADI DESEMBA MWAKA 2016 HAKUNA MWANAFUNZI ALIYE PATA MIMBA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI UPONERA.
AIDHA AMEWATAKA WAZAZI KUTOWAACHIA MAJUKUMU WATOTO WAKATI WA KIPINDI CHA KILIMO KWANI HALI HIYO INAPELEKEA WATOTO HAO KUJIHUSISHA NA VITENDO VIOVU WAKIWA WADOGO.
MWISHO .
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.