Na . Yuster Sengo
Wafugaji wametakiwa kufuga kisasa ili kupunguza migogoro na kujipatia faida ya kufuga mifugo kwa tija
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa maliasili na utalii Mohamed Omary Mchengelwa alipotembelea banda la Halmashauri ya wilaya ya Ulanga kwenye viwanja vya Nane Nane mjini Morogoro ili kujionea maonesha kwenye banda hilo
Mh Mchengelwa amesema kuwa mifugo inatakiwa ifugwe kwa kuwafungia ng”ombe na sio kuwaacha wakizurula hovyo jambo linalopelekea migogoro kati ya wafugaji ,wakulima pamoja na maeneo ya hifadhi ya wanyamapori
Waziri Mchengelwa amesema kuwa kama Ng”ombe watafugwa vizuri watakuwa na afya njema,watatoa maziwa ya kutosha lakini pia nyama yake itakuwa nzuri na mfugaji atapata faida kubwa kwenye ufugaji wake
Maonwesho ya nane nane yanafanyika mjini Morogoro kwa kanda ya mashariki inayobebwa na kauli mbiu isemayo “Vijana na Wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula”
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.