NA FATUMA MTEMAGA
Ujenzi wa miundo mbinu ya barabara ya kiwango cha lami na daraja la Mzingizi lililopo kata ya Sali wilayani Ulanga Mkoani Morogoro unatarajia kukamilika tarehe ishirini na tano mwezi wa kumi mwaka 2018 ili wananchi wa kijiji cha Isyaga waweze kupata huduma za msingi kwani huduma hizo zilisimama kutoka kana na miundo mbinu hiyo ya daraja kusombwa na maji wakati wa mvua za masika za mwezi wanne mwaka huu.
Akizungumzia ukamilishwa wa ujenzi huo mkuu wa mkoa wa Morogoro ndugu Kebwe Steven Kebwe amewataka wakandarasi wanaojenga miundo mbinu hiyo kukamilisha kwa wakati ifikapo tarehe 25 mwezi wa kumi mwaka 2018 kwani hali ya hewa kwa Wilaya ya Ulanga sio ya kuridhisha hii ni kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Hata hivyo dk.Kebwe aliwataka wakazi wa Sali kutoa ushirikiano katika shughuli za maendeleo kwani maendeleo hayana itikadi ya chama hivyo wasiingize mambo ya siasa kwenye maendeleo ili kumuunga mkono mh.Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania dk.John Pombe Magufuli anavyosimamia shughuli za maendeleo bila kuangalia itika ya chama wala ukabila.
“Maendeleo hayana itikadi ya chama kila mtu anataka maendeleo kwani Zahanati si tunatumia wte,barabara,maji na shule tunatumia wote sasa wakandarasi nimeongea na nyie mmenielewa sasa nataka ufanye kazi kwa haraka mkamilishe ujenzi huu, leo una bahati sana na kama mkienda tofauti nawachukulia hatua na kwa mkoa wa Morogoro tusingewapa tena kazi”.Alisema Kebwe
Pia mkuu wa mkoa amewataka wakandarasi hao wa kampuni ya Luqma Construction Com.Ltd na Mmeto Construction Com.Ltd kuwalipa vibarua kwa bei elekezi ya viwango vya serikali ambapo kutwa moja ni wanalipwa shilingi elfu saba badala ya shilingi elfu kumi na tatu ambayo ni viwango vya serikali hivyo ametoa siku 5 kuandaa gharama walizo kuwa wanalipa vibarua hapo awali na ukamilishaji wa ujenzi huo na kuwasilisha ofisi ya mkuu wa mkoa saa mbili kamili asubuhi.
“Nataka nikija hapa tarehe ishirini na tano nikute barabara hii imeisha na daraja likamilike na sio kufanya uzembe halafu mvua zianze kunyesha iharibu tena na kuhusu hawa vijana wetu nataka muwalipe kwa makubaliano ya viwango vya bei elekezi ya serikali na kuwalipa kiholela holela tu haiko hivyo nataka barabara hii iishe sitaki uzembe na watu wa Tanroads nataka mfanye haraka kufanyia vipimo sampuli zinazoletwa ofisini kwenu.
Aidha mkuu wa nkoa amewataka wakazi wa kijiji cha Isyaga na Sali kutunza miundombinu ili huduma za msingi ziendelee ili iweze kupitika wakati wa mvua za masika na kiangazi kwani wapo watu wanapoteza maisha ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa hivyo kama miundo mbinu hiyo haitatunzwa serikali haitaleta fursa zingine katika maeneno hayo.
Ndugu zangu wakazi Sali na Isyaga mfanye kazi hii kwa vizuri kabisa na uaminifu kwa bidii kama ninavyowaona muwe na uzalendo ili barabara hii ikamilike hakuna kujiachia mimi katika ziara yangu nikija naongea na wafanyakazi mimi sitakuja kuongea na viongozi mkuu wa wilaya au mkurugenzi hata huko nilikotoka sikuongea na wakurugenzi wala wakuu wa wilaya hapana mmepata bahati ya kupata serikali inawajali sasa sitaki mfanye uzembe nataka nikija tarehe ishirini na tani barabara hii iiishe.
katika ziara yake mkuu wa mkoa amekagua miradi ya maendeleo kwa mkoa wa Morogoro inayotekelezwa na ilani ya chama cha Mapinduzi {CCM} ambapo mradi wa barabara kilometa nane unatakiwa kujengwa kwa kiwango cha lami na daraja la mto mzingizi lijengwe kwa umakini kutokana na daraja hilo kusombwa na maji mwezi wa nne wakati wa mvua za masika.
Mradi wa barabara ulianza kutekelezwa mwaka 2015/2016 kwa mkataba wa shilingi milioni mia nane thelathini na nne laki nne sitini na mbili elfu mia mbili na sabini na tano{834,462,275.60} unaotekelezwa na kampuni ya Mmeto Construction Com ambapo mradi huu ulisimama kwa mwaka mzima baada ya daraja linalounganisha sehemu mradi ulipo kusombwa na mafuriko lakini kwa sasa mkandarasi amekamilisha kuimarisha tabaka la juu kwa kuchanganya kifusi na saruji hivyo kazi zilizobaki ni kuweka matabaka ya lami na kujenga mifereji na ifikapo mwezi wa kumi mradi huo utakamilika.
Ziara ya mkuu wa mkoa wa Morogoro dk. Kebwe Steven Kebwe katika wilaya ya Ulanga imekamilika kwa kugakua miradi ya maendeleo katika kata ya Ruaha kijiji cha Sali,Iyaga kwa kugagua ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilometa nane pamoja na daraja la Mzingizi ili kutekeleza ilani ya chma cha Mapinduzi .
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.