NA ERNEST BALUA
VIJANA WILAYANI ULANGA MKOANI MOROGORO WAMETAKIWA KUUNDA VIKUNDI VIDOGO VIDOGO KWAAJILI YA KUJIPATIA MIKOPO MBALIMBALI ILI KUJIENDELEZA NA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO .
HAYO YAMESEMWA NA AFISA MAENDELEO YA JAMII BWANA EDWIN MASANJE NA KUONGEZA KUWA OFISI YA MAENDELEO YA JAMI INAJARIBU KUTOA ELIMU HASA KWA VIJANA NA WAJASILIAMALI MBALIMBALI ILI KUWEZA KUPATA MIKOPO HIYO AMBAPO KWA MWAKA 2016-17 OFISI HIYO IMETOA ZAIDI YA SHILING MILIONI KUMI KWA VIJANA.
HATAHIVYO BAADHI YA VIJANA NA WAJASILIAMALI HAO WAMESEMA KUA, KUTOKUA NA ELIMU YA KUTOSHA KUHUSIANA NA MIKOPO, KUNAWAFANYA KUTOELEWA NI SEHEMU GANI WANAWEZA KUCHUKUA MIKOPO HIYO NA HIVYO KUISHIA KUJIINGIZA KWENYE SHUGHULI AMBAZO ZISIZO RASMI.
AIDHA WAMEONGEZA KUWA WANAHITAJI MIKOPO MBALIMBALI ILI KUWEZA KUJIENDELEZA NA SHUGHULI ZA KIJAMII KAMA KULIMA BUSTANI NA KUFUGA SAMAKI ILI KUJINUFAISHA NA PIA KUJIPATIA AKIPATO.
SAMBAMBA NA HAYO BWANA EDWINI MASANJE AMBAYE NI AFISA MAENDELEO YA JAMII AMETOA WITO KWA VIJANA AMBAO NDIO NGUVU YA TAIFA KUENDELEA KUFANYA KAZI ILI KUEPUKANA NAMASUALA YASIO YA MSINGI IKIWEMO UTAPELI NA WIZI NA KUWASIHI VIJANA KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA KUCHUKUA MIKOPO
PIA KWA UPANDE WA MWAKA 2016-17 VIJANA WENGI WAMEWEZA KUJITOKEZA KUCHUKUA MIKOPO, AMBAPO WALIUNDA VIKUNDI VIDOGO VIDOGO NA KUWEZA KUPATIWA FEDHA ZA KUENDELEZA MITAJI YAO
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.