Ulanga
na Fatuma Mtemangani
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga nd.Yusuf Semuguruka ameipongeza Kata ya Iragua kua nimiongoni mwa kata iliyofanya vizuri katika ujenzi wa vyumba vya madarasa,viti pamoja na meza kwa wanafunzi watakao jiunga na kidato cha kwa kwanza kwa mwaka 2018.
Akizungumza katika ziara ya kutembelea ujenzi wa madarasa hayo nd.Semuguruka amesema kua kata ya Iragua imeonyesha matumaini ya kutimiza lengo kwa kila kata ambayo ina upungufu wa madarasa ifikapo tarehe 8/1/2018 kwa shule za sekondari tano wilayani humo.
Hata hivyo amewaahidi viongozi wa kata kwa kushirikiana na waheshimiwa Diwani wa kata husika viongozi wa vijiji na vitongoji kuwa kama watafanya kazi nzuri na kwa wakati Halmashauri itatoa msaada wa mabati,nondo za kuweka kwenye madirisha pamoja na sementi kwa ajili ya ujenzi huo.
Aidha viongozi hao wameishukuru Halmashauri kwa msaada watakaoupata na kuahidi kuwa hadi ifikapo tarehe 8/1/2018 ujenzi huo utakuwa umekamilika.
Katika ziara hiyo mkurugenzi ameambatana na kaimu mkuu wa wilaya nd.Abraham Mwaikwira,Afisa elimu sekondari Menard Lupenza,Afisa Maendeleo ya jamii Mohamed Atiki pamoja na mlezi wa kata husika.

Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.