Na.Yuster Sengo
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh.Martin Shigella ameipongezaHalmashauri ya wilaya ya Ulanga kwa kupata hati safi kwa mwaka wa fedha 2019-2020
Akizungumza kwenya mkutano maalumu wa baraza la madiwani la halimashauri ya wilaya ya ulanga wakati wa kuwakilisha ripoti ya mthibiti na mkaguzi mkuu wa serikali (cag) kwa mwaka wa fedha 2019/2020 na utekelezaji wa maagizo ya kamati ya bunge na serikali za mitaa (laac) Mh.Shigella amewapongeza viongozi waliomtangulia kwa kufanikisha halmashauri za mkoa wa Morogoro kupata hati safi
“Hata hivyo nawapongeza viongozi walionitangulia kwenye mkoa huu kwa kufanikisha kupata hati safi kwa halmashauri zote tisa za mkoa huu,ushirikiano wao ndiyo uliosababisha kupatikana kwa hati hizo safi kwa mwaka huu wa fedha”Amesama Mh Shigella
“Kupata hati safi tusibweteke halafu mwakani mkaja kupata changamoto katika hesabu zenu za mwaka na kusababisha kupata hati chafu au yenye mashaka “Ameongeza Mh Shigella
“Kama Halmashauri mnatakiwa kuwa timu moja ,lakini hapa mnaonekana mna ushirikiano na hata baraza lenu linaonekana lipo huru na linaibua hoja za msingi na zinapata majibu”Amesema Shigella
Aidha amewataka waheshimiwa madiwani kuhakikisha hoja hazijitokezi katika miaka inayokuja ili kuweza kukwepa kupata hati chafu au yenye mashaka
“Uongozi wa Halmashauri wekeni mkakati wa jinsi ya kulipa madeni hayo na mpeleke suala hili kwenye kamati ya fedha na mjadili jinsi gani mtalipa au kulipwa madeni hayo
Hata hivyo amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Ulanga Mh.Ngollo Malenya pamoja na timu yake kuweka msisitizo katika suala la madeni yanayodaiwa na halmashauri yalipwe kwa wakati ili kuweza kuongeza mapato ya Halmashauri
“Mpaka kufikia Mei tuna asilimia 59 ya mapato na tuna mwezi mmoja tu umebaki kumaliza mwaka wa fedha wa serikali hivyo tupo chini sana ingawa DC,Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi walinipa sababu ,ila naahidi kuzifanyia kazi sababu hizo ili kila mmoja anayestahili kulipa kodi afanye hivyo na hatimae kupandisha mapato ya Halmashauri”Amesema Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh.Martin Shigella
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Mh.Ngollo Malenya amesema kuwa Halmashauri ifanye kazi kwa bidii na hati safi iliyopatikana kwa mwaka huu wa fedha isiwafanye mlewe sifa
“tuendelee kufanya kazi kwa bidii ili tuendelee kupata hati safi hata kwa mwaka mwingine wa fedha “Amesema Mh.Malenya
“Sina shaka na utendaji kazi wenu kwasababu wote bado tunatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi hivyo tuendelee kushirikiana na kufanya kazi kwa bidii kwa maslahi mapana ya wilaya yetu”Ameongeza Mh.Malenya
Naye kaimu katibu tawala mkoa wa Morogoro Bw.Leopard Ngirwa ameishukuru Halmashauri kwa kutulia na kujadili na kufikia muafaka wa Hoja za mkaguzi mkuu wa serikali
Aidha ameongeza kuwa suala hili limefanikiwa kutokana na ushirikiano mzuri kati ya uongozi wa Halmashauri na waheshimiwa madiwani
“Niwaombe madiwani mbebe dhamana ya mnaowawakirisha ,panapotokea kulega lega kwenye mambo ya hapa halmashauri basi msimamie vizuri ili mambo yaende sawa .”Ameongeza Bw.Ngirwa
Hata hivyo mkuu wa MKoa wa Morogoro Mh.Martin Shigella amesema atahakikisha anapita kwenye vijiji vyote vya Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga kuhakikisha kero zote zinazowakabili wananchi kwenye maeneo yao zinatatuliwa kwa wakati ili kuwawezesha wananchi hao kujikita katika shughuli za uzalishaji mali
mwisho
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.