Na .Yuster Sengo
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe.Martin Shigela ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga kuendelea kuimarisha mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya halmashauri ikiwa ni pamoja na kuhakikisha watu wote wanaodaiwa na Halmashauri wanalipa madeni yao.
Mhe. Shigela amesema hayo wakati wa kikao cha baraza maalum la hoja ya mkaguzi mkuu wa serikali Wilayani Ulanga ambapo kikao hicho kimehudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Mkoa wa Morogoro ili kujadili Ripoti ya Mkaguzi wa Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 .
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro amewaagiza Wakuu wa Idara mbali mbali Wilayani Ulanga kutoa ushirikiano kwa madiwani na Mbunge wa jimbo la Ulanga pindi wanapotaka ufafanuzi wa changamoto mbali mbali zinazowakabili Wananchi ili kuboresha Maendeleo Wilayani Ulanga.
Kwa upande wake Mbunge wa Wilaya ya Ulanga Mhe.Salim Alaudin Hasham amesema kuwa asilimia themanini ya Wananchi wa Wilaya ya Ulanga ni Wakulima hivyo katika kuhakikisha wanaboresha sekta hiyo ya kilimo, Ofisi ya Mbunge ilinunua Matrekta matatu na kuyapeleka kwa Wananchi ambayo yamesaidia kulima Zaidi ya Hekari 700 za Wananchi na Wakulima Wamekua wakilipia asilimia kumi ya gharama za kulimishia mashamba yao.
‘’Wilaya yetu inategemea sana kilimo,ofisi ya mbunge ililiona hilo na kununua trekta tatu ambapo wakulima huwa wanahangia kiasi kidogo sana cha asilimia kumi ili yaweze kuwasaidia kulimia mashmba yao’’Amesa Mh. Salim
Pamoja na hayo pia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Bi.Saida Mahugu amekiri kuyapokea maagiizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa na kuanza kuyafanyia kazi mara moja ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kama kuna mapungufu basi hayatajirudia tena
‘’Ninayapokea maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa na ninaahidi kwa kushirikiana na CMT yangu tutayafanyia kazi maagizo hayo na kuhakikisha hakuna mapungufu mengine yatakayo jitokeza tena ‘’ Amesema Ndg Mahugu
mwisho
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.