Na. Yuster Sengo
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh. Loata Ore Sanare amemtaka mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga Ndg. Jonas Mallosa kuhakikisha pesa zote zinazokusanywa na halmashauri kuingizwa benki kwa utaratibu wa elektroniki kabla ya akuzifanyia matumizi
Akizungumza katika baraza maalum la hoja ,Mh Sanare amesema kuwa ,mkurugenzi hakatazwi kutumia pesa hizo kama anavyotaka ila anatakwa kufuata utaratibu kabla ya kufanya matumizi yoyoyta
“ Haunyimwi kutoa na kutumia uavyotaka wewe ila katika aeneo mengi ndani ya halmashauri zetu wakata hela juu kwa juu wanawapatia shida vijana wale wana tukusanyia fedha kwa sababu maelekezo yanatoka kwa mkurugenzi,maelekezo yanatoka kwa DT,maelekezo yanatoka kwa Yule mwingine “Amesema Mh. Sanare
Aidha ameongeza kuwa kutokana na usimamizi mbovu wa fedha za halmashauri kw mwaka wa fedha 2017/2018 halmasahuri ya wilaua ya Ulanga ilipata hati isiyoridhisha hali ambayo siyo nzuri kwa ustawi wa halmashauri yetu
“Ninatambua kwa hati hiyo isiyoridhisha ndiyo maana mmekezana na hatimae mwaka wa fedha wa 2018/2019 mmekazana na hatimae mmepata inayoridhisha”Ameongeza Sanare
Hata hivyo ameongeza kuwa mashaka yaliyosababisha halmashauri kupata hati isiyoridhisha ni kutokana na usimamizi mbaya wa mapato ya ndani yanayokusanywa na halmashauri ambapo zaidi ya shilingi bilioni moja ilihojiwa juu ya usimamizi wake
Amesema kuwa kutokana na hati ambayo halmashauri imepata kwa mwaka huu wa fedha , inaonyesha kuwa kumekuwepo na usimamizi wa rasilimali za umma unaoridhisha
Hata hivyo amesisitiza kuwa ni wajibu wa baraza la madiwani na menejimenti kwa ujumla kuyalinda mafanikio ya mwaka uliopita ili wasije wakarudi tena nyuma
“Baraza hili liwe kali na menejimenti msikie ushauri kutoka kwa baraza la madiwani ,msije mkarudi huko ambapo tulipata hati isiyoridhisha “Ameongeza Mh. Sanare
Mh. Sanare ametoa wito kwa baraza la madiwani kuhakikisha wanaendeleza utendaji kazi mzuri kwa kuepuka utendaji wa mazoea na usio zingatia taratibu ili kuepuka hoja zisizop kuwa za lazima
Aidha amewataka waheshimiwa nmadiwani kuhamasisha na kuhakikisha wananchi wanalipa kodi kama ambavyo wamekuwa wakilipa ili fedha hizo zije kwaajili ya kutatua changamoto zote zilizopo ndani ya halmashauri ya Ulanga
“Maeneo mengine madiwani wengine ndion shida , wanahamasisha wananchi wasilipe kodi,hii ni shida sana na kwa bahati mbaya sana tuazo taarifa za madiwani wa kata hizo wanaofanya mambo kama hayo hatutawavumilia “Amesema Sanare
Mwisho
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.