Na.Yuster Sengo
Mkuu wa mkoa wa morogoro Kebwe Steven Kebwe amewaomba wa kazi wa tarafa ya lupiro kulinda na kutunza kituo cha afya Lupiro kwani kituo hicho kinafaida kubwa ya kutoa huduma za kiafya katika tarafa hiyo
Akizungumza katikamkutano wa wananchi mara baada ya kukagua kituo hicho ambacho kipo katika hatua za mwishoni kukamilika,mkuu wa mkoa amesema kuwa majengo hayo ambayo ni chumba cha upasuaji,wodi ya akina mama wajawazito,chumba cha kuhifadhia maiti,maabara pamoja na nyumba ya mganga imegharimu shilingi milioni mia nne pesa iliyotolewa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Joseph Magufuli
“Majengo hayo yote hayo yaliyojengwa pale ni ya kisasa kabisa na imegharimu shilingi milioni mia nne na pesa hii imetolewa na Rais Magufuli kwaajili ya kuboresha sekta ya afya nchini”Amesema Dkt Kebwe.
“Na pale kwenye kile chumba cha upasuaji kumefungwa vifaa vya kisasa kabisa ambavyo pia vitasaidia sakafu isigandie uchafu kabisa kama tunavyofahamu katika chumba cha upasuaji huwa kuna uchafu mbalimbali”Ameongeza Dkt Kebwe
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa sula la elimu bila malipo limeendelea kupewa kipaumbele ambapo tarafa ya Lupiro imepewa shilingi Milioni 270 kwaajili ya ujenzi wa shule ya sekondari katika tarafa hiyo
Aidha amewataka watendaji na wenyeviti wa vijiji kusimamia kwa ukaribu suala la majitolea kwa wananchi ili ujenzi huo uende kwa haraka kwani ifikapo mwezi wa saba mwaka huu ,majengo hayo ya sekondari yanatakiwa kuanza kutumika
“Mmeanza vizuri hamasa,na kazi mliyofanya jumamosi ni nzuri sana kwahiyo muendelee na hivyo hivyo ili watoto wetu waanze kutumia madarasa hayo mapema iwezekanavyo”Amesema Dkt Kebwe.
Aidha amemuomba diwani wa kata hiyo ya lupiro kuandaa ratiba itakayowafanya wannchi kutajua kuwa ni zamu ya kijiji Fulani kufanya majitoleo ili wajitokeze kwa wingi katika kufanya majitoleo hayo ambayo yatasaidia kumaliza ujenzi kwa wakati.
Hata hivyo amewakumbusha watendaji pamoja na wananchi kuwa ifikapo tarehe 30/6 /2019 pesa hizo zakutekeleza mradi wa kujenga sekondari Lupiro zitzrudishwa serikalini kama zitakuwa bado hazijatumik
“Hiyo ni sheria, kama fedha zitakua hazijatumika hadi kufikia tarehe 30/6 basi pesa hizo zitzrudishwa ,kumbukeni kuwa hii ni sheria na ipo wazi hivyo ni juhudi zetu za majitoleo zitakazo tusaidi kumaliza mradi huu kwa wakati”Ameongeza Dkt Kebwe
Aidha wananchi wa Tarafa ya Lupiro wamekubaliana kutumia nguvu ya pamoja ili kumaliza kazi ya ujenzi wa sekondari ya Lupiro na kuanza kutumika na wanafunzi ifikapo mwezi wa saba mwaka huu.
Mwisho
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.