Na yuster sengo
Mkuu wa mkoa wa morogoro Dkt KEBWE STEVEN KEBWE amewataka wananchi mkoani humo kuilinda miundombinu iliyopo ili kuunga mkono jitihada za mh rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania Dkt JOHN POMBE MAGUFULI za kuleta maendeleo nchini.
Akuzungumza katika kikao maalum cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri wa pauline wilayani ulanga Dkt KEBWE amesema kuna changamoto ya baadhi ya wananchi wasio waadilifu kuhujumu miundombinu ikiwemo ya barabara na kuwataka wananchi kuacha tabia hiyo.
Hata hivyo Dkt KEBWE amemwagiza mkuu wa wilaya ya ulanga Bi NGOLLO MALENYA akishirikiana na kamati ya ulinzi na usalama wilayani hapa kuwakamata na kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kuhujumu miundombinu ya daraja la magufuli lililopo katika kijiji cha kivukoni ili iwe fundisho kwa wengine.
“Miundombinu hii ni sisi wote kuilinda, lipo hilo tatizo katika mkoa wa morogoro. tushirikiane kuilinda miundombinu hii inatusaidia sana”. Dkt KEBWE
Dkt KEBWE aliendelea kueleza kuwa “lakini wapo wengine wanahujumu kwa maksudi, sidhani mtu na akili yake timamu anaweza kwenda kunyofoa hizo nati mchezo huu wa kilevi levi huu wameanza kufungua taa kwaiyo tusaidiane kwa njia hiyo, hatuwezi kuwa na polisi kila sehemu tushirikishe mifumo yetu ulinzi shirikishi lakini pia wananchi wapo, mgambo wapo tusaidiane kulinda miundombinu hii” dkt KEBWE.
Katika hatua nyingine Dkt KEBWE steven kebwe amekemea tabia ya baadhi ya wanasiasa wanaotumia siasa kuhamasisha wananchi kuhujumu miundombinu iliyopo ambapo amwagiza mkuu wa wilaya ya ulanga bi ngollo malenya kuwafatilia watu hao na kuwachukulia hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.
Amesema kitendo cha baadhi ya wanasiasa kukaa vikao na kujadili mikakati ya kuhujumu miundombinu ni kupoteza muda kwani hawata fanikiwa na badala yake watakumbana na nguvu ya dora na kuchukuliwa hatua huku serikali ikiendelea kujenga nchi kwa manufaa ya tanzania nzima.
“Hujuma za namna hiyo ambazo zipo organized crime( mipango ya hujuma) kwamba ngoja tujipange bhana tuhujumu mradi huu kwaiyo kila mtu anaingia kwa staili yake wanapoteza muda tu”
Katika kikao hicho maalumu cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya ulanga kilichoitishwa na mkuu wa mkoa wa morogoro kimehudhuriwa na waheshimiwa madiwani wa kata zote 21 za wilaya, kamati ya ulinzi na usalama, vyombo vya habari na vyama vya siasa huku ajenda kuu ikiwa ni mkuu wa mkoa kuwasilisha taarifa ya uchunguzi wa ubadhilifu wa fedha kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 2 ikiwa ni utekelezaji wa maagiza kutoka tamisemi.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.