ULANGA
Na Thabit Mpoma
Wakazi wa wilaya ya ulanga mkoani morogoro wameombwa kuendelea kutunza mazingira na kupuka kuchoma misitu ili kukabiliana athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.
Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nanungu tarafa ya Mwaya wilayani Ulanga katika ziara ya kujitambulisha na kusikiliza kero mbalimbali za Wananchi mkuu wa wilaya ya ulanga Mh Ngollo Malenya amesema kwamba atapambana na yoyote atakayetuhumiwa au kujihusisha na uchomaji wa misitu wilayani humo.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya huyo ameeleza kwamba ameshatoa matangazo kupitia Radio Ulanga na tayari amewaandikia barua viongozi wa vijiji pamoja na wataalamu wa kilimo kueleza sheria na taratibu za uandaaji wa mashamba kwa kutumia moto ili kupambana na athari hizo.
Pia amewaagiza viongozi wa vijiji kutolifumbia macho swala hilo kwakuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa kiongozi yoyote atakaeenda kinyume na sheria au taratibu hizo za utunzaji wa mazingira.
Katika hatua nyingie mkuu wa wilaya huyo ametoa rai kwa wakazi wa kijiji hichocha nanungu kujiunga kwa wingi katika mpango wa taifa wa bima ya afya chf kwakuwa unaweza kuwapunguzia gharama zamatibabu hasa pale wanapopata rufaa ya matibabu ya juu zaidi.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.