ULANGA
NA FATUMA MTEMANGANI
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Bi. Ngollo Malenya amewataka watumishi wote waliopo katika Idara mbalimbali kufanya kazi kwa weledi kwa kutoa huduma kwa jamii na kuacha kufanya kazi kwa mazoea hali itakayopelekea kurudisha nyuma maendeleo ya Wilaya.
Bi. Ngollo ameyasema hayo wakati alipokutana na watumishi wote wilayani hapa katika ukumbi wa Halmasahauri wa Pauline kuzungumza nao na kukemea vikali suala la majungu miongoni mwa wafanyakazi kwani hata livumilia katika uongozi wake hivyo upole wake usiwe kigezo cha kutotoa maamuzi kwa mtumishi.A
Aidha amwetoa wito kwa watumishi kuzingatia muda wa kuingia kazini na kutoka kazini pamoja na kufuata sheria ya mavazi ya kiutumishi kwani serikali haitamvumilia mtumishi atakae kiuka sheria na taratibu za kiutumishi.
“Upole wangu usiwe kigezo cha kunichukulia poa siku zote mtu mpole ana kitu ndani yake naomba tusicheze na kazi mimi ni mcha mungu sana ndiyo mana sipendi majungu na sipendi mtu aje ofisini kwangu kwa ajili ya kumsemea majungu mfanyakazi mwenzake hapana sijaumbwa hivyo na sitakuwa hivyo nichokitaka uje ofisini kwangu tushirikiane kufanya kazi na ndiyo maana mh.Rais ameniteuwa kwakuwa ameniamini na nyinyi mfanye kazi kwa weledi na kushirikiana ili tulete maendeleo wilayani hapa.Alisema Ngollo Malenya”.
Hata hivyo mkuu wa Wilaya ameahidi kutoa ushirikiano katika idara ya Elimu kwa kwa shule za msingi na sekondari kwa kuwahimiza wazazi na walezi kujitolea kufyatua matofali kwa kila kijiji kuwa na benki ya tofali ili zisaidie katika ujenzi wa vyumba vya madarasa,matundu ya vyoo,maabara pamoja na nyumba za walimu ambapo imekuwa ni changamoto kubwa kwa kila Halmashauri nchini.
Pia ameanza ziara yake ya kuzunguka kila kijiji wilayani Ulanga kwa ajili ya kuzungumza na wenyeviti wa vijiji hivyo amewataka wasiwe maafisa Ardhi kwa kugawa Ardhi bila mpangilio na badala yake wafuate sheria na taratibu zilizowekwa za ugawaji wa Ardhi ambapo kiwango chake ni hekali hamsini.
Aidha ameongeza kwa kulitaka jeshi lapolisi wilayani Ulanga kuchukua maamuzi ya haraka kwa kutenda haki kwa raia na mali zao pale wanapopeleleza kesi ili kusiwe na mrundikano wa kesi mahakamani na mahabusu gerezani kwa kufuata sheri za utumishi wa uma.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.