Na .Yuster Sengo
Mkuu wa wa wilaya ya Ulanga Ngollo Malenya amewataka watendaji wa kata ya Iragua kuwa wakali kwa wananchi wa kata hiyo ambao hawashiriki katika majitoleo na ikiwezekana wawatoze faini ili waweze kukujitokeza wanapohitajika kwaajli ya majitoleo
Kauli hiyo imekuja mara baada ya Mkuu wa wilaya kuambiwa na watendaji wa kata hiyo kuwa muamko wa kufanya majitoleo umekuwa haupo na wananchi hawajitokezi kabisa pamoja na kwamba wanapewa taarifa mapema kuhusu majitoleo
Aidha mkuu wa wilaya ameongeza kuwa kwa wananchi wasiojiyokeza wapigwe faini kwani kusipofanyika chochote inawavunja moyo na wengine wanaojitokeza kwenye majitoleo
“Muwapige faini wale wote wanao kaidi kufanya majitoleo,msikae kimya tu na kuwangalia kwani mkifanya hivyo inawavunja moyo na wengine wanao jitahidi kufanya majitoleo”Amesema Ngollo
Kutokana na hali hiyo ya kusuasua ya majitoleo , mkuu wa wilaya alitaka kujua ni lini majengo hayo yatakamilika ili yaanze kutumika na wanafunzi
Akijibu swali hilo fundi mkuu Killian Mandaki amesema kuwa kama kutakuwa na ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wananhi na vifaa vyote vikafika kwa wakati majengo hayo yatamalizika na kukabidhiwa baada ya wiki tatu
“Mimi ninanguvu kazi ya kutosha ,kama wananchi watafanya majukumu yao ya kujitolea kwa wakati na nikapata vifaa vyote kwa wakati,basi naahidi kukabidhi majengo haya baada ya wiki tatu tu”Ameongeza fundi mkuu Mandaki.
Hata hivyo mkuu wa wilaya Ngollo Malenya amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inaleta pesa za kujenga madarasa na kumalizia maboma ili kutoa huduma bora kwa wananchi hivyo ni jukumu letu kufanya majitoleo ili miradi hiyo imalizike na ianze kutumika kwa wakati
Aidha amesisitiza suala la chakula mashuleni na kusema kuwa shule zote zitoe chakula kwa wanafunzi ili kuweza kuongeza ufaulu mashuleni.
“Suala la chakula mashuleni halina mjadala,watoto hawa wanatakiwa kupata chakula wanapokuwa shuleni hivyo ni jukumu letu kulisimamia hilo ili watoto wapate chakula “Amesema Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngollo Malenya
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya huyo amesema kuwa atapita tena katika kata ya Iragua baada ya wiki hizo tatu ili kujihakikishia kama jingo hilo limeisha na kwa kiwango kinachotakiwa kama alivyo ahidi fundi mkuu anayesimamia ujenzi wa madarasa hayo
mwisho
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.