Na.Yuster Sengo
Mkuu wa wilaya ya Ulanga Mh. Ngollo Malenya leo mei 18,2022 amezindua kampeni ya zoezi la utoaji chanjo ya polio kwa watoto chini ya miaka mitano
Uzinduzi huo umefanyika katika hospitali ya wilaya ya Ulanga ambapo zoezi hilo la utoaji chanjo utafanyika nyumba kwa nyumba kwa wataalamu wa Afya kupita katika nyumba hizo kutoa chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano
“kwahiyo natoa wito kwa walezi na wazazi wote kuhakikisha kama kuna mtoto wa miaka mitano anapata chanjo hiyo kwa ajili ya kulinda afya zao”Amesema Mh Mkuu wa wilaya Ngollo Malenya
Aidha ameongeza kuwa Serikali kupitia wizara ya afya imeagiza watoto wote chini ya umri wa miaka mitano kupatiwa chanjo ya polio kuwafanya watoto kuwa na Afya bora
“Serikali kupitia wizara ya Afya imeagiza zoezi hili la chanjo ya polio kwa watoto wote chini ya miaka mitano ili kuongeza kinga za mwili kwa watoto na kuhakikisha tunaondoa maambukizi hayo ya kirusi hicho cha polio kwa watoto wote nchini”Ameongeza Mh.Ngollo
Mkuu wa wilaya ameongeza kuwa chanjo hiyo imezinduliwa na itafanyika kwa siku nne kuanzia tarehe 18 /05/2022 hadi tarehe 23/05/2022 ikiwa na lengo la kuimarisha afya za watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Aidha ameeleza kuwa mtoto yeyote hazuiliwi kurudia kupata chanjo hiyo kwa wakati mwingine kwani sababu ya kurudi kuchanja ni kupunguza ukali wa virusi vya polio na kuongeza kuwa zipo njia nyingi za maambukizi hayo kwa kupitia njia ya kula na hata njia ya kupumuiliana.
Sambamba na hayo Mh Ngollo amesema kuwa watoto wanapaswa kuzingatiwa katika zoezi zima la kupatiwa chanjo ya polio ili kuendelea kuwa na afya njema pamoja na kinga ndani ya miili
Naye mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Ulanga Dk Ally Mjema amesema kampeni hii imeanza rasmi baada ya kuzinduliwa na mkuu wa wialya na yeye pamoja na timu yake wapo tayari kutekeleza maagizo hayo kutoka wizara ya Afya kwa kiwango cha juu
MWISHO
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.