Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya UlangaYusuf Daud Semguruka amefanya ziara ya kustukiza katika mnada wa kijiji cha mbuyuni ili kujionea makusanyo ya ushuru yanavyofanyika.
Akiwa katika mnada huo mkurugenzi amejionea jinsi makusanyo ya ushuru yanavyofanyika kwa kutumia mashine na kuona changamoto mbalimbali katika mnada huo.
Moja ya changamoto aliyoikuta ni ya kukosekana kwa banio hivyo ameahidi kulitengeneza la muda ili liweze kusaidia kwa kipindi hiki.
Aidha kwa upande wao wafanyabiashara wanaofanyabiashara zao katika mnada huo wamesema kuwa mnada huo unawasaidia kwani kwasasa hawaendi tena mbali kama vile mnada wa Itete na Malinyi.
Hatahivyo wamesema kuwa wanaiomba serikakali iwatatulie changamoto walizonazo katika mnada huo ikiwemo ya ukosefu wa maji na uzio katika mnada huo.
Licha ya changamoto walizonazo wafanyabiashara hao wamempongeza mkurugenzi wa halmashauri ya Ulanga kwa kufika kutambua changamoto zao kwani wamesema kuwa wakitembelewa na kiongozi kama huyo basi wanaamini hata changamoto zao zitafahamika na kutatuliwa kwa wakati.
Mnada huo unawasaidia wananchi kuanzia maeneo ya wilaya ya Kilombero mpaka Ulanga pamoja na maeneo yote kuanzia Lupilo na vitongoji vyake kwa kupata huduma mbalimbali za uuzwaji wa ng’ombe na bidhaa nyinginezo.
Mbali na hilo mnada huo pia unasaidia kuongeza mapato kwa halmashauri ya wilaya Ulanga pamoja na kijiji cha Mbuyuni kwa kupokea ushuru kutoka kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara mnadani hapo.
Mwisho
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.