NA YUSTER SENGO
Wakazi wa kitongoji cha kazimoto na Mbela Kitonga wamepatiwa mafunzo ya jinsi ya kuhifadhi na matumizi sahihi ya fedha za fidia zinazotokona na kupisha mradi wa kampuni ya Tanzagraphite
Akizungumza kwa nyakati tofauti katika vitongoji hivyo Afisa uhusiano wa kampuni hiyo Bwana Benard Mihayo amesema kuwa kampuni hiyo haitapenda kuona wanufaika wa mradi huo wakiztumia fedha hizo vibaya hivyo wameamua kutoa elimu hiyo il iweze kuwanufaisha wanufaika hao
“kampuni yetu haitapenda kuona watu wanafanya matumizi mabaya ya fedha ambayo baadae yatawafanya kuwa maskikini,hivyo kila mnufaika apange matumizi mazuri ili aweze kujiinua kiuchumi”Amesema Mihayo
Hata hivyo Bwana Mihayo ameongeza kuwa baadhi ya mandeleo yatakayofanywa na kampui hiyo katika kitongoji cha Mbela Kitonga ambapo ni sehemu ya watakao hamishiwa watu watakao pisha mradi epanko ni pamoja na kujnga shule yenye madarasa 13,nyumba za walimu 13,pamoja na kujenga kituo cha afya ambacho kitakuwa na wodi ya wanawake,wanaume,watoto pamoja na nyumba 3 za wauguzi
Aidha ameongeza kuwa baada ya kumaliza kutoa elimu hii,hatua itakyofuata ni kwa mwanasheria wa kampuni hiyo kufika katika vitongoji hivyo na kusaini mikataba ili alipo ya fidia yaingizwe kwenye akaunti za wanufaika hao
Hata hivyo muwezeshaji aliyehudhuria mafunzo hayo Bi Paulina Mwakuli amewataka wanufaka wa mradi kupanga mpango ya matumizi ya fedha hizo na kutoa kipaumbele kwa matumizi muhiu
“nawasisitiza kupanga mipango sahihi ya matumizi ya fedha zenu namkiwa mnapanga make kwa pamoja baba,na mama na kila mnapotoa pesa benki mshirikishane ili kila mmoja ajue kiasi kiichotumika na kiasi kilichobaki”amesema Bi Paulina
Naye manager wa Bank ya CRDB Bw.Mustafa Hoza amewaomba wanufaika hao wa mradi kuondoa wasiwasi juu ya fedha zao zitakazohifadhiwa bank na kwamba pesa hizo ziko salama na makato ya kila mwezi hayatakuepo kwa wanufaika hao
Katika mafunzo hayo kuliambatana na upimaji wa vvu kwa hiari kwa wanufaika hao ili kujua hali ya afya zao na muitikio wake likua mkubwa kwani watu wengi walijitokeza kwaajili ya zoezi hilo la upimaji kwa hiari
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.