ULANGA
Na
Fatuma Mtemangani
Chama cha Wana Sheria WanawakeTtanzania(TAWLA)kimetoa msaada wa usafiri aina ya baiskeli thelathini kwa wasaidizi wa Sheria katika Vijiji kumi ili waweze kuwafikia wananchi kwa urahisi.
Akizungumza baada ya kukabidhi baiskeli hizo kwa wasaidizi hao kaimu mkuu wa Wilaya ambae ni Afisa Tawala Wilayani Ulanga Bi Hulka Hamisi amewashukuru TAWLA kwa msaada huo kutokana na baadhi ya wananchi Wilayani Ulanga kutojua sheria hasa juu ya haki na wajibu katika umilikishwaji wa ardhi.
Hata hivyo Bi hulka amewataka wanasheria wasaidizi kutunza vyombo hivyo vya usafiri ili viweze kuwasaidia katika vijiji vyao kwa kufanya kazi kwa moyo,kujituma na kushirikiana kwa kutoa elimu kwa jamii ili kupunguza migogoro ya ardhi ndani ya wilaya ya ulanga.
kwa upande wao wanasheria wasaidizi wamewashukuru TAWLA kwa kuwapatia usafiri kwani utawarahisishia utendaji kazi katika vjiji vyao kwa kuifikia jamii kwa wakati hivyo wanaahidi kufaya kazi kwa weledi na kujituma ili kufikisha elimu waliyoipata kwa kutatua migogoro ya ardhi kwa ngazi ya kijiji,kata na tarafa.
Pia wameahidi kushirikiana na viongozi wa Vijiji,Kata na Tarafa kwa kupitia mikutano yao kutoa elimu juu ya haki na wajibu katika umilikishwaji na urasimishaji wa ardhi kwa wanawake Wilayani Ulanga kwani kwa kufanya hivyo itaondoa ile dhana ya kubaguliwa kwa mtoto wa kike kwa kutomilikishwa ardhi.
Mradi wa uhamasishaji wa wananchi juu ya haki na wajibu kwenye umilikishwaji wa ardhi,upimaji na urasimishaji ardhi uko Mkoani Morogoro katika Wilaya mbili ambazo ni Kilombero na Ulanga,na kwa Wilaya ya Ulanga mradi huo upo katika kijiji cha Igota,Chikuti,Ketaketa,Iragua,Mbuga,Chilombora,Iputi,Nkongo,Mdindo pamoja na Ebuyu ni vijiji ambavyo wanasheria wasaidizi wamepatiwa mafunzo.
Mwisho.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.