ULANGA
Na Fatuma Mtemangani
Wafugaji Wlayani Ulanga Mkoani Morogoro wametakiwa kufuata sheria,haki na taratibu za ufugaji wa kisasa ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima kati ya wafugaji na wakulima katika maeneo wanayoishi ili kuongeza kipato.
Hayo yalizungumzwa na mkimbiza Mwenge kitaifa ndugu Charles Kabeho wakati wa kutoa ujumbe wa mwenge wa Uhuru baada ya kukabidhiwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga katika kata ya Iragua ikitokea Halmashauri ya wilaya ya Malinyi na kukabidhi vyeti kwa wafugaji zaidi ya kumi na madume ya ng’ombe bora aina ya Mpwapwa ili wafugaji waweze kumiliki ng’ombe wachache kwa faida kubwa pia kuondoa migogoro baina ya wakulima na wafugaji kwa Wilaya ya Ulanga.
Ndugu zangu wafugaji niwaombe mzingatie sheria na taratibu za ufugaji bora kwa kuondoa migogoro isiyo lazima,na haya madume ya ng’ombe mlioyopewa mkayatunze vizuri itawaletea mabadiliko makubwa sana lakini pia mtapata kipato kikubwa ambacho mtaweza kuendesha maisha yenu na kizazi chenu cha sasa na cha baadae na hamta kuwa na malumbano yeyote hasa kwa Viongozi wa Wilaya ya Ulanga pamoja na Wananchi wa Ulanga,Alisema Kabeho.
Ndugu Kabeho aliongeza kuwa Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2018 umesisitiza sna masuala ya Elimu hivyo wazazi na walezi wana jukumu la kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni ili waweze kuongeza uelewa wanapofundishwa ambapo kwa sasa ni mikoa miwili tu kwa Tanzania nzima ikiwemo Njombe na Kilimanjaro ndiyo inawapatia chakula wanafunzi shuleni kwa zaidi ya asilimia tisini.
Hata hivyo aliwahasa wazazi na walezi kutokwepa jukumu la kuwanunulia sare za shule watoto wao hasa shule za Msingi ambao wengi wao wanavaa sare zilizotoboka na mashati yasiyo na vifungo hii ni tofauti sana na shule za Sekondari.
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 pia aliwasihi wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao kwa kufuatilia mahudhurio yao shuleni na kupitia madftari yao ili kujua maendeleo ya mtoto wake na pia kujua kama ana matatizo na baadhi ya masomo na hatimae aweze kuwasiliana na mwalimu wa somo husika na kumuelewesha tatizo alilokuwa nalo mtoto wake ili apate uelewa mzuri na aweze kutimiza ndoto zake.
Aidha amewasisitiza wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao waliohitimu kidato cha nne ambao wamefaulu kwenda vyuo vya ufundi ikiwemo VETA na vyuo vya Maendeleo ya Jamii wawapeleke kwa wakati wakapate ujuzi ambao utawasaidia kujiajiri au kuajiriwa ili kuendana na dhana ya Nchi ya Viwanda,kuboresha uchumi na kuleta maendeleo endelevu kwa kufikia uchumi wa kati.
Kuna baadhi ya wazazi na walezi mmekuwa hamna ushirikiano na walimu na wala hamfuatilii kabisa maendeleo ya mtoto wako na kuna wengine hawatekelezi majukumu yao kwa watoto wao na kuaznia sasa wazazi mchangie chakula tu shuleni ili watoto wetu wawe na nguvu ya kusoma na waweze kufaulu vizuri,na kama mzazi hatatekeleza wajibu wake huyo hatutamfu hata kidogo,nataka kila kiongozi asimamie majukumu yake katika idara yake ili Ulanga iweze kusonga mbele kielimu kama inavyofanya vizuri kwa sasa.
Pia aliwaasa jamii ya wafugaji kuwapeleka watoto shule kwani ni haki yao na ifikapo mwaka 2019 wahakikishe watoto wote wanakwenda shule wakapate elimu ambayo ni ufunguo wa maisha yao na serikali imeendelea kuwekeza katika sekta ya elimu kwa kujenga vyumba vya madarsa,nyumba za walimu pamoja na maabara kwa shule za sekondari katika kata zote za wilaya ya Ulanga.
Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2018 umekimbizwa katika halmashauri ya Wilaya ya Ulanga tarehe 27 mwezi wa 7 mwaka 2018 ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ambapo umepitia miradi kwa kuzindua,kuona miradi ya Afya,Elimu,Viwanda vya Nafaka,Jumuiya ya watumiaji Maji pamoja na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa soko la mazao Mahenge Mjini na kuitaka Halmashauri kumalizia miradi isyokamilika kwa wakati.
Mwenge wa Uhuru kwa wilaya ya Ulanga umekimbia kilometa 230 na umetembelea miradi tisa yenye thamani ya shilingi bilioni 1.966 ambapo milioni mia moja na arobaini na saba ilitoka serikali kuu,milioni ishirini na tano zilichangiwa na Halmashauri,milioni miamoja na arobaini na mbili walichangia wananchi na bilioni 1.651 wamechangia wadau wa maendeleo wa wilayani Ulanga.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.