Na. Yuster Sengo
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga Mh. Nassoro Kihiyo amesema kuwa mapato ya halmashauri ya wilaya ya Ulanga yameshuka kutoka asilimia mia moja sitini (160%) kwa robo ya kwanza hadi kufikia asilimia sitini na nne (64%)kwa robo ya tatu
Akisoma hotuba katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani, Mh.Kihiyo amesema kuwa katika robo ya kwanza mapato yalikuwa ni shilingi 894,761,000 sawa na asilimia 161% ya makusanyo yote na robo ya pili halmashauri ilikusanya SHILINGI 456,896,631 sawa na asilimia 86% na kwa robo ya tatu halmashauri imekusanya jumla ya shilingi 339,964,925.76 sawa na asilimia 64.2 ya maksanyo yote
“Kwa kuangalia tu mwenendo wa mapato wa mapato tangu robo ya kwanza hadi robo ya tatu ni dhahiri kuwa mapato ya halmashauri yameshuka “Amesema Mh. Kihiyo
Hata hivyo ameopngeza kuwa mapato hayo yanashuka kwasababu mbali mbali ikiwemo halmashauri hiyo kukumbwa na mafuriko yaliyosababisha madhara katika makazi ya watu ambapo nyumba 32 zimezingirwa na maji ,miundombinu ya barabara imeharibika na hekali 3404 za mazao ya mahindi ,mpunga na ufuta zimeathiriwa
Aidha ameongeza kuwab sababu nyingine ya kushuka kw mapato ni pamoja na kuchelewa kwa msimu wa mazao hususani ufuta na kuwepo kwa ugonjwa hatari wa homa ya mapafu uliosambaa duniani kote ikiwemo Tanzania unaosababishwa na virusi vya corona
“pamoja na ugonjwa huo kuenea duniani kote na kufikia hapa Tanzania lakini hadi sasa halmashauri yetu haijaripoti kisa chochote cha ugonjwa huo,aidha tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu mlezi wa viumbe vyote aweze kutunusuru na ugonjwa huu” Ameongeza Kihiyo
Hata hivyo amewaomba madiwani kuendelea kutoa elimu ju ya ugonjwa huu kwa wananchi nwa kata zao ili wasiendelee kuathirika kisaikolojia na kiuchumi
“Tuendelee kumuunga mkono raisi wetu kwa kuondoa hofu wananchi na kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kujenga uchumiwetu wan chi na halmashauri yetu na kuongeza mapato”Mh. Kihiyo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga
Mh.kihiyo ameendelea kuwashauri wananchi wa wilaya ya Ulanga kupanda mazao ya mizizi hususani mihogo pamoja na kulima mahindi katika maeneo yote yenye miinuko na mpunga maeneo ya mlimani ili wapate mazao ya kutosha ya chakula na biashara
Hata hivyo ameongeza kuwa halmashauri hiyo inatakiwa kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato na kuwa wabunifu katika kubuni vyanzo vipya na vyenye uhalisia na tija vitakavyoleta maendeleo na ustawi wa watu wa Ulanga na halmashauri kwa ujumla
“Ili halmashauri yetu iweze kujiimarisha kiuchumi,tunawashauri wananchi kulima mazao ya biashara kama vile korosho,pamba,ufuta karangamiti na kokoa ili kuongeza kipato cha mwananchi mmoja mmoja na hatimae kupandisha mapato ya halmashauri”Amemalizia Mh.Kihiyo
Mwisho
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.