Na.Yuster Sengo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Mh.Edson Solly amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuruhusu maonesho ya nane nane kufanyika kwani inawasidia wananchi kujifunza teknolojia mpya nakupata bidhaa kwa bei nafuu
Akizungumza mara baada ya kutembelea na kujionea bidhaa na Teknolojia mbalimbali zinazopatikana katika banda la Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Mh.Solly amesema kuwa amefurahi kushiriki kwenye maonesho hayo ya nane nane na kujifunza mambo mbalimbali
“kwa kifupi nimefurahi sana kushiriki kwenye maonesho haya kwani yamefana sana na kama unavyoona watu wamekuwa wengi na inaonekana ni namna gani watu walikuwa na hamu sana haya maonesho
“kwa mwaka huu maonesho haya yameandaliwa kwa muda mfupi sana lakini naona wataalam wamejitahidi kwa uwezo wao ila kwa mwakani naamini Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga tutajipanga vizuri zaidi
Naye katibu wa Mbunge wa Ulanga Thomas Dafa akizungumza kwa niaba ya Mbunge wa Ulanga mh.Salim Alaudin Hasham amesema kuwa maonesho haya imekuwa ni fursa kubwa kwa wajasiliamali wa Ulanga kutangaza bidhaa zao na kujiinua kiuchumi kwani Ulanga kuna vitu vizuri vyenye ubora
“ Tunawakaribisha wageni kuja kujionea vitu vizuri vinavyopatikana Ulanga ,na ni jambo zuri kushiriki maonesho haya ili kujitangaza maana tukijifungia tu wenyewe watu hawawezi kujua kama Ulanga kunapatikana vitu vizuri kwahiyo ni lazima watu waje kuona hapa ili baadae waje Ulanga kujionea kwa uhalisia”Amesema Dafa
Hata hivyo Dafa amempongeza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri,Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na wataalam wa Halmashauri kwa kujipanga vizuri katika maonesho hayo
“kwakweli nimpongeze mkurugenzi,mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na wataalam wote kwa kujipanga vizuri kama ambavyo unaona banda letu linatembelewa na wageni wengi,siyo wa Ulanga tu hadi wan je ya Ulanga wanakuja kuona vitu mbali mbali ambavyo vipo hapa”Ameongeza Dafa
Kwa kumalizia Mh. Solly pamoja na Katibu wa Mbunge Bw.Dafa wamewasihi wakazi wa Ulanga kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa siku ya 23/8/2022 na kuwapa ushirikiano mkubwa makarani waliopewa jukumu la kuhesabu watu na makazi ili serikali iweze kupata idadi kamili ya Wananchi na kupanga bajeti kulingana na Takwimu hizo
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.