Na.Yuster sengo
Mwenyekiti wa tume ya madini nchini Profesa Idris Kikula amesema hakuna mchimbaji yeyote wa madini atakae bainika kutorosha madini na akawa salama ,nakuagiza watumishi wote wa madini wawe waadilifu katika kusimamia na kutekeleza maagizo hayo ya serikali
Profesa Kikula amesema hayo wilayani Ulanga mkoani Morogoro katika ziara yake ya kutembelea migodi mbali mbali pamoja na kuzungumza na wachimbaji wadogo.
Akiwa katika migodi ya madini Epanko,Profesa Kikula amewataka wachimbajikuhakikisha wanayatumia maduka yaliyoanzishwa na serikali kuuza madini yao na sikuyatorosha.
"tulimuahidi Rais kuwa hatutatorosha tena madini,na tulimuomba atupunguzie kodi,Rais akafanya hivyo sasa hakuna sababu ya kutorosha madini, tufanye kazi kwa uadilifu na tutumie maduka yaliyoanzishwa ili kuuza madiniyetu"Amesema Profes Idris.
"Serikali inawaona wachimbaji wadogo kama marafiki lakini ,lakini urafiki huu unaishia pal ambapo watatorosha madini na ukitorosha hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yako"Ameongeza Profesa Idris.
Awali akitoa taarifa ya madini ,Afisa madini mkazi mkoani Morogoro Emanuel Shija amesema hadi sasa tayari leseni 400kati ya elfu tatu zimefutiwa usajili baada ya wamiliki wake kushindwa kuziendeleza.
Ziara ya mwenyekiti wa madini wilayi Ulanga ina lengo la kukagua shughuli mbalimbali za uchimbaji wa madini pamoja na kuzungumz na watumishi wa sekta ya madini
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.