NA.YUSTER SENGO
Naibu waziri wa madini Mh. Dotto Biteko ameruhusu shughuli za uchimbaji madini kuendelea katika wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro baada ya kufungiwa kuendelea na kazi kwa takribani miezi mitano
Akizungumza na wadau wa madini pamoja na wananchi ,mh.biteko amesema kuwa walilazimika kufunga migodi hiyo sababu ya udanganyifu na kutofata taratibu za ulipaji kodi
“Tulikuja hapa mwezi wa sita tukaenda hadi epanko tukaangalia shughuli zinazoendela ,hatukulizishwa ,tukarudi tena mwezi wa saba tarehe kumi,tukalazimika kufunga migodi hiyo ili tuweze kujipanga maana kodi nyingi sana zinapotea kwenye sekta ya madini’’amesema biteko
Aidha ameongeza kuwa zama zimebadilika sana sasa hivi,kwa kuwa serikali ya awamu ya tano inajitahidi sana kuzuia rushwa hivyo mtu akifanya kazi kwa uadilifu anaweza kutajirika
“Badilikeni fateni utaratibu,na ni bora ukachelewa kuanza kufanya kazi kuliko kuanza kufanya kazi kinyume cha utaratibu “amesema Biteko
Aidha ameongeza kuwa pamoja na kuruhusu kwa shughuli za uchimbaji kuendelea,wizara ya madini imezindua ofisi ya madini iyakayokuawa inashughulikia masuala yote yanayohusu madini wilayani hapa
Hata hivyo ameongeza kuwa wizara ya madini haitamani kufunga mgodi hata mmoja ila kutokana na ukiukwaji wa taratibu wizara inalazimika kufikia hatua hiyo
“Wizara ya madini haitamani kufunga mgodi hata mmoja kwakuwa migodi hiyo inasaidia kuendesha nchi kwa kupitia kodi ila mazingira yanasababisha kufikia kwa hatua hiyo,ameongeza Mh. Biteko
Migodi ya madini ilifungiwa rasmi kuendelea na kazi za uchimbaji tarehe 10/7/2018 na leo tarehe 14/12/2018 migodi hiyo imefunguliwa kwa sharti la wachimbaji kukamilisha malipo yao kwa awamu walizojiwekea na hivyo kuanza kazi ya uchimbaji rasmi
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.