Na.Yuster Sengo
Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ulanga leo tarehe 8/4/2019 imekabidhi vitambulisho 2000 vya ujasiriamali kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ulanga Bw. Jonas Mallosa avisimamie na kuviuza kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kabla ya tarehe 15/04/2019 ambapo ndiyo mwisho wa zoezi la kusambaza vitambulisho hivyo
Akizungumza katika kikao kazi cha maafisa tarafa,watendaji wa vijiji,watendaji kata pamoja na wakuu wa idara,katibu tawala wilaya ya Ulanga Bw. Abraham Mwaikwira amesema kuwa zoezi hili la uuzaji wa vitambulisho hivi inatakwa ushirikiano baina ya ofisi ya mkurugenzi na ofisi ya mkuu wa wilaya na siyo kazi ya mtu mmoja tu
Aidha ameongeza kuwa kutokana na kauli ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Magufuli kuwa atawawajibisha wakuu wa mikoa na wakuu wa wialaya kama wasipouza na kumaliza vitambulisho na hivyo hivyo ,ofisi y mkuu wa wilaya atawawajibisha watendaji watakao fanya mzaha kwenye uuzaji wa vitambulisho hivyo
“tulimsikia Rais akizungumza kule Mtwara kuwa atawawajibisha wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya atakaozembea kuuza vitambulisholakini kabla ya hapo na sisi tutachukua hatua yakuwajibisha watendaji wazembe”Amesema Mwaikwira
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga Ndg.Jonas Mallosa amewataka watendaji kusimamia na kuuza vitambulisho hivi kwa uwezo wao wote ili kuiwe na sababu yoyote ile ya kuwajibishana
“kesheni mkiuza vitambulisho hivi na niwakumbushe tu nitatafuna kuanzia makatibu tarafa na kushuka chini kama tu hamtazingatia maagizo haya kuhusu vitambulisho “Amesema Mallosa
Hata hivyo amewataka watendaji hao kugawa vitambulisho hivi kwa wajasiriamali wadogo na anae pewa kitambulisho asidaiwe tena kodi nyingine
Vitambulisho hivi,ni kati ya vile vitambulisho 670000 vilivyochapishwa na Rais Magufuli na kugaiwa kwa wajasiriamali wadogowadogo nchi nzima
mwisho
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.