Na.Yuster Sengo
Katibu tawala wilaya ya ulanga bwana abrahamu mwaikwira amemtaka mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya ulanga mh.furaha lilongeli na baraza lake la madiwani kuwa wakali na kuchukua hatua dhidi ya watendaji walioshindwa kutekeleza majukumu yao katika maeneo yao.
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani bwana mwaikwira amesema ofisi ya mkuu wa wilaya imesikitishwa na hatua ya kuwahamisha vituo vya kazi baadhi ya watendaji waliosababisha kuganda kwa mifuko ya saruji iliyopelekwa katika maeneo yao kwa lengo la kutumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa.
“Naomba baraza hili la madiwani liwe na maamuzi magumu,kwa zile sehemu ambazo sementi zimeganda,maafisa watendaji wachukuliwe hatua na siyo kuhamishiwa sehemu nyingine,”amesema mwaikwira
Bwana mwaikwira amesema ofisi ya mkuu wa wilaya imeona hatua ya kuwahamisha vituo vya watendaji hao haikuwa sahihi na badala yake hatua za kisheria zinapaswa kuchukuliwa dhidi yao ili iwe fundisho kwa wengine na kuliomba baraza la madini wilayani hapa kulitazama suala hilo na kuchukua hatua stahiki.
Kauli hiyo ya bwana mwaikwira inakuja wakati huu ambapo halmashauri ya wilaya ya ulanga inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa 23, viti 2624 na meza 2636 ambapo madiwani wametakiwa kushughulikia changamoto hii hadi mwishoni mwa mwezi ujao uli kuwapa nafasai wanafunzi 2733 waliofauli elimu ya msingi kujiunga na elimu ya sekondari januari mwakani.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya ulanga mh.furaha lilongeli amesema kuwa yapo maagizo waliyotoa katika ziara ya kamati ya fedha,uchumi na mipango kuwa kwa sehemu ambazo kumepelekwa vifaa hivyo vya ujenzi wa vyumba vya madarasa na havijatumika ,basi vitahamishwa na kupelekwa sehemu nyingine kwenye uhitaji
Aidha amewaomba waheshimiwa madiwani,na viongozi wa siasa kijumla kuacha kuonyesaha utashi wa kisiasa kwenye kuleta maendeleo bali wafanye kazi ushirikiano ili kuharakisha kasi ya maendeleo
“Niwaombe viongozi wenzangu,tuache kabisa kuonyesha utashi wa kisiasa katika kata zetu,tuweke itikadi za kisiasa pembeni ,tufanye kazi kwa kushirikiana ili kuharakisha maendeleo katika kata zetu na wilaya kiujumla”amesema Mh Lilongeli
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.