Na Yuster Sengo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya y Ulanga Mh. Furaha Fadhili Lilongeli ,ametoa taarifa rasmi kwa baraza la madiwani kuhusu kujiuzulu kwa aliyekua diwani wa kata ya Msogezi Mh.Menrad Chipeta
Akisoma taarifa ya kujiuzulu ya diwani huyo, Mh Lilongeli amesma kuwa alipokea barua ya kujiuzulu ya diwani huyo na kwa mujibu wa taratibu na sheria ni lazima atoe taarifa kwenye kikao cha baraza la madiwani
”Nilipokea barua kutoka kwa aliyekua diwani wa kata ya Msogezi kwa tiketi ya Chadema ,Mh.Menrad Chipeta akiomba kujiuzulu na kujiunga na Chama cha Mapinduzi kwa madai kuwa akiwa chama cha Chadema anapata tabu sana kuhudumia wananchi wa kata yake”Amesema Lilongeli
Aidha ameongeza kuwa mara baada ya kupokea barua hiyo,nay eye akamuandikia barua kwa katibu mkuu TAMISEMI ili kumjulisha kuwa kuna kata iliyoachwa wazi kutokana na aliyekua diwani wa kata hiyo kujiuzulu wazfa wake huo
“Baada ya kupata barua hiyo na mimi nikaandika barua kwa katibu mkuu ili kumjulisha kuhusu suala la kujiuzulu kwa diwani wa Msogezi na kata hiyo ipo wazi kwa sasa ili utaratibu mwingine ufuatwe:”Amefafanua Mh. Lilongeli
Hata hivyo ameongeza kuwa baada ya kutoa taarifa hiyo kwa katibu mkuu TAMISEMI,kitakachofata ni kazi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ambaye ni msimamizi wa uchaguzi kufanya utaratibu unaofuata.
Mwisho
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.