Ulanga
Idara ya afya wilayani iulanga mkoani Morogoro imefanikiwa kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto vinavyotokana na uzazi kutoka vifo 80 hadi 60 kati ya laki moja kwa mwaka 2016/017.
Akizungumza na Ulanga Fm mganga mkuu wa wilaya bwana Rajabu Risasi amesema mafanikio hayo yametokana na uboreshwaji wa huduma ya mama na mtoto ikiwemo upatikanaji wa vifaa na madawa kwenye vituo vya kutolea huduma.
Ameongeza kuwa licha ya mafanikio hayo idara ya afya inakusudia kuwajengea uwezo wa utendaji watumishi kutoka 50% hadi 60% kwa wilaya ya Ulanga ili kuendelea kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya hasa kwa akina mama wajawazito na watoto
Aidha akizungumzia kuhusu hali ya maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi na ugonjwa wa Kifua kikuu wilayani ulanga Dkt Risasi amesema kwa upande wa VVU maambukizi yamepungua kutoka 2.7% hadi 2% huku akibainisha kwa upande wakifua kikuuu kutoka wagonjwa 49 hadi 40.
Pia mganga mkuu akielezea kuhusu tatizo la ugonjwa wa akili amesema idara ya afya imefanikiwa kupunguza tatizo hilo kutoka 9.5% hadi 8% kwa mwaka 2016/2017
Kwa mujibu wa mganga mkuu Idara ya afya wilayani ulanga inaendelea kutekeleza mpango wa kuboresha huduma zake kupitia vituo 26 vya kutolea huduma ambavyo Hospital 1,vituo vya Afya 2 pamoja na Zahanati 23..ili kuendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Na Fatuma Mtemangani.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.