Ulanga
Kitengo cha maendeleo ya jamii Wilayani Ulanga mkoani Morogoro imewataka kamati ya afya ya kata pamoja na wahudumu wa afya kutoa elimu hasa kwa jamii ya wafugaji juu ya kujikinga na maambukizi mapya ya ukimwi.
Hayo yamebainishwa mratibu wa Ukimwi wilaya ya Ulanga Bi. Leah Ndama wakati alipowasilisha ripoti ya utekelezaji ya kitengo cha Ukimwi kwa kipindi cha robo ya tatu kwa 2016/2017.
Bi. Leah amesema kua kupitia kitengo cha ukimwi wilaya ya Ulanga imetekeleza mpango wa upimaji endelevu katika vituo vya kutolea huduma ambapo akina mama wajawazito wapatao 1078 wamepima kwa hiari.
Aidha kuhusu taarifa ya vyeti vya kuzaliwa idara yake imefanikiwa kutekeleza zoezi la ufuatiliaji na ugawaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto waliopo katika vijiji mbalimbali wilayani humo isipokuwa kijiji cha Mtimbira na malinyi kutokana na wahusika ambao ni jamii ya wafugaji kuyahama makazi yao
Pia Amesema Idara kupitia kamati zake imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa elimu inayohusu masuala ya VVU na Ukimwi ili kuwawezesha kutambua namna sahihi ya kuishi na maambukizi pamoja na kujikinga na maambukizi mapya ya ukimwi
Amewataja wadau hao kuwa ni pamoja na Baraza la waislam Tanzania wilaya ya Ulanga BAKWATA ambao wamejenga kituo cha elimu kwa watoto, CHAMA CHA WAKRISTO KKKT, MORAVIAN, ROMAN KATOLIKI, CHAMA CHA WASIOONA, NGOs, CBOs, USAD,WAVIU,pamoja na BORESHA AFYA.
Na Fatuma Mtemangani.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.