ULANGA
NA Fatuma Mtemangani
Mradi wa kupambana na uharibifu wa mazingira wilaya ulanga mkoani morogoro kilorwemp umefanya jitihada kubwa ya kulinda na kuokoa bonde la kilombero kwa kulinda uharibifu wa wanyama unaotokana na baadhi ya wananchi wanaoishi katika mipaka ya hifadhi.
Akizungumzia uharibifu huo afisa wanyamapori mkuu bwana Jeradi Kauzeni wakati alipopewa nafasi kwenye baraza la madiwani kuzungumzia kazi zinazofanywa na idara ya wanyamapori amesema kua ameishukuru kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya ulanga kwa ushirikiano wao wa kufuata na kusimamia sheria ya wanyamapori iliyowekwa na serikali kwa vijiji husika ili kunusuru uharibifu wa wanyama pori unaofanywa na baadhi ya vijiji ambavyo vinavyo pakana na hifadhi.
Hata hivyo bwana Kauzeni ameongeza kua mradi wa kilorwemp umefanya jitihada kubwa ya kutoa elimu kwa jamii juu ya kuwalinda wanyama pori kwa kufanya mikutano kwa vijiji vinavyo pakana na ardhi ya wanyama pori hivyo amewataka wananchi wafuate sheria,kanuni na taratibu ya kumiliki ardhi.
Aida amesema kua mradi kwa sasa umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kupambana na uharibifu wa mazingira hivyo upo kwenye harakati za kujenga ofisi ya iluma katika kijiji cha kivukoni ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi.
Maadhimisho ya siku ya ardhi oevu nchi hufanyika kila mwaka na kauli mbiu ya mwaka huu inasema kuwa ustahimili na uendelezi maeneo ya ardhi oevu kwa ustawi wa miji.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.