Ulanga
Na
Fatuma Mtemangani
Kituo cha Afya cha Lupiro wilayani Ulanga kwa sasa kinatarajia kukamilisha ujenzi wa majengo mawili ikiwemo jengo la kuhifadhia maiti pamoja na jengo la akina mama wajawazito na watoto walio chini ya miaka mitano lengo likiwa ni kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto kwa wilaya ya Ulanga.
Akizungumzia ukarabati huo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri Ndugu Yusuph Semguruka amesema kua ujenzi huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni mia nne fedha kutoka tamisemi ili kutoa huduma mbalimbali za afya katika kituo hicho cha afya.
“Ujenzi huo umefanyika kwa kujenga upya majengo hayo na sio kukarabati kutoka wodi ya kujifungulia,sehemu ya akina mama kujisubiria kujifungia,chumba cha kuhifadhia maiti kwa sababu chumba cha awali tutaweka huduma nyingine,kuweka huduma ya maji safi na salama na kubadilisha mfumo wa umeme hivyo tunajua sekta ya afya nchini ina changamoo nyingi sana hivyo serikali hii ya awamu ya tano imeitazama kwa jicho la tatu sekta hii ya afya kwa kuweka mazingira mazuri ikiwemo kuongeza majengo mapya kwa ajili ya akina mama wajawazito na watotot walio chini ya miaka mitano ili kuokoa vifo vya akina mama na watoto”.alisema Semuguruka.
Hata hivyo Mkurugenzi ameongeza kua wakazi wa Lupiro wamefurahia kuongezeka kwa majengo hayo kwani utasaidia usalama wa akina mama wajawazito na watoto kwa awali walikuwa wakipata shida sana ya uhaba wa majengo ya kujifungulia kwa kukaa nje huku wakinyeshewa mvua wakatia wa masika na kupigwa na jua wakati wa kiangazi hali ilyokuwa ikipelekea kukemewa na baadhi ya wauguzi.
“Ndugu zangu wakazi wa Lupiro mmepata bahati ya kupata majengo mazuri na makubwa kwa ajili ya kupata huduma hii muhimu ya afya sasa nataka muyatunze majengo haya ili huduma ziendelee kwa sababu mama zetu wanateseka sana na watoto ambao ni nguvu kazi ya Taifa letu wanapoteza maisha mimi nitakuwa nakuja kuyakagua haya majengo na kama haukufuatwa utaratibu wa kuyatunza fursa zingine zikitokea hatutazileta hapa lupiro aswa jamani.”alisema Semguruka.
Halmasahuri ya wilaya ya Ulanga kupitia sekta ya afya imefanikiwa kudumisha bima ya afya CHF iliyoboreshwa zaidi kwa ajili ya wananchi wenye kipato cha chini kwa kuwapatia vifaa tiba,kwa kila zahanati,vituo vya afya pamoja na hospitali ya wilaya na huduma kwa wazee pia zinapatikana bila kikwazo chochote.
Kwa upande wa wakazi wa Lupiro wao walifurahia sana majengo hayo hivyo wamemuomba Mkurugenzi kuwaboreshea na maeneo mengine ikiwemo eneno la mapokezi na chumba cha kuchukulia dawa kwa wagonjwa wan je ili waweze kupata huduma bora na kwa wakati.
Lengo la ujenzi wa kituo cha afya Lupiro ni kuboresha huduma ya afya na kusogeza huduma hiyo karibu na wananchi wake hivyo mpaka kukamilika kwa ujenzi huo umegharimu jumla ya shilingi milioni mia nne kutoka Tamisemi.
Mwisho.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.